Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,493
- 4,770
USHAANZA KUBORONGA.
1)kocha alikusaliti,peke yako ukacheza.
Ukashinda mikakati,ukiwa na wale wenzako.
Zikashinda harakati,na likapona anguko.
Mbona waanza boronga,tofali limekushinda.
2)bawabu usiwamini,ndo mana wakudanganya.
Ni vitisho mtaani,walaini kama nyanya.
Ngoja wakupige chini,ndipo uanze kuminya.
Mbona waanza boronga,tofali limekushinda.
3)mbona twarudi zamani,zile zama za foleni.
Aibu hadi mjini,watu jipanga dukani.
Ni uongo w jukwani,utatokea puani.
Mbona waanza boronga,tofali limekushinda.
4)kama ulidhani yai,hakika ukufikiri.
Sema okoa uhai,wasizinduke mangiri.
Ona waanza furai,kushinda kwako kukiri.
Mbona waanza boronga,tofali limekushinda.
5)nguvu hazina wakati,mikono itaongea
Mashariki hadi kati,mwenyewe utajonea.
Bwana wa mahaqamati,atashindwa kukimbia.
mbona waanza boronga,tofali limekushinda
Shairi:USHAANZA KUBORONGA.
Mtunzi:Idd ninga tengeru arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com