Umoja wa mataifa (UN) kupitia shirika lake la afya duniani (WHO) huadhimisha wiki ya kimataifa ya nenda kwa usalama barabarani kila mwaka. Asasi za kiserikali na binafsibhualikwa katika kuadhimisha wiki hiyo kila mwaka.
Organization against transport accidents (ORATA) Ndio asasi (NGO) pekee iliyo jitokeza kuadhimisha wiki hiyo. Maadhimisho yalianza Tar. 8 na yanakamilika tar. 14. Ya mwezi 5 mwaka 2017.
Lengo la maadhimisho haya ni kumkumbusha kila mtumiaji wa barabara juu ya usalama wake na juu ya usalama wa watumiaji wengine wa barabara na mali.
Mafanikio haya kwa namna yake yamefanikiwa kukuwa mafundisho mengi na muhimu yamewafikia watu mbalimbali hasa wa Dar es salaam na pia nje ya DSM kwa wale wanaotumia mitandao ya kijamii.
Jana Tar. 12, ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa ORATA kufanya maadhimisho haya.
Maadhimisho haya yalipambwa na maandamano ya Raia na wanafunzi wa shule za sekondari na msingi ili kutoa hamasa kwa umma kuzingatia sheria na kanuni za matumizi bora na sahihi ya barabara. Maandamano yaliianzia stendi ya mabasi ya mikoani (Ubungo) kuelekea chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) kupitia barabara ya Morogoro na Mabibo. Msafara uliongozwa na askari wa usalama barabarani, Misululu ya pikipiki, Brass band na maandamano ya watu.
Ujumbe wa mwaka huu ni Save lives, slowdown
Pia neno Slowdown limewekewa hash tag ilikuweza kuunganisha juhudi za watu wote duniani katika kupaza sauti juu ya usalama barabarani