Umungu wa uongozi tanzania

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Ukiwa ni kiongozi wa Tanzania unakuwa kama kamungu fulani hivi.Si unajua huwezi mlazimisha "mungu"kufanya kama hajaamua yeye?Je,huu "umungu"unatoka wapi?(labda katiba na uoga wetu).

Mtu anachukua fomu anakua mgombea,anajipitisha kwa unyenyekevu kuomba awe rais ATI ili apate nafasi ya kuwatumikia,mnamchagua,mkishamchagua anabadilika,hataki tena kuwasikiliza na kuwatumikia.Amesha kua mungu hapo!

Hapo unaanza kusikia"vimungu wengine"wasema,"piga tu,lazima wapigwe,hee!! sasa tumechoka,nami nasema lazima wapigwe" hapo rais yupo kimya.Mnamwambie,mkuu tunapigwa,tunauwawa,tunapigwa mabomu ebu unda tume ya kimahakama tumjue mtesi wetu!!!Mnapiga kelele,yeye anasema tumechoka! Sasa kama mmechoka si mturudishie dola yetu tuwape wenye nguvu? we mtu umechoka,then unang'ang'ania tuu,si uondoke?

Watanzania tunateswa na "umungu" wa viongozi wetu,hawatusikilizi tena? Tuhakikishe tunauondoa huu umungu wa kiuongozi kupitia njia yeyote kwa manufaa yetu,ya watoto na wajukuu zetu!
"wonga ni dhambi kubwa kuliko zote",G.Lema (mb)
 
Back
Top Bottom