Bunge kama muhimili linatakiwa liendeshwe kufuatana na sheria na kanuni . Majukumu ya Bunge katika kuisimamia serikali ni kupitia miswada kujadili na kuipitisha kuwa sheria .
Kujadili na kupitisha bajeti ya matumizi ya serikali
1. Iwapo bajeti yote ya Nchi huandaliwa na Wizara ya Fedha kisha kujadiliwa Bungeni na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kisha kupitishwa au kukataliwa.
Bajeti ya Nchi ndiyo inaweka wazi na kuidhinisha mipango na matumizi gani yatafanyika kwa mwaka husika wa fedha kwa kutumia fedha za serikali.
2. Kwa kumbukumbu zilizopo za Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 sijasikia ama kuona kama Serikali ilitenga Kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya kununua Ndege kama tulivyoshuhudia zikiingia hivi karibuni, Ndege mbili aina ya Bombardier ambazo tunaambiwa zimenunuliwa kwa fedha taslimu sio mkopo. Labda kama fedha za kununulia ndizo tulikopa
3. Sioni mahali ambapo Bil kumi za kujenga mabweni zilipojadiliwa na bunge na kuidhinishwa,vivyo hivyo kwa Bil 10/= za nyumba za Magereza na Bil 10/= za hospitali Fulani.
Sijawahi kuwasikia wabunge wakihoji haya ndani ya bunge. Mambo muhimu yanayotakiwa kutolewa matamko na Bunge tunasikia tu kwenye mitandao
4. Tumeshuhudia wabunge walipozidiwa nguvu na mtu mmoja (ns) katika kutekeleza wajibu wao wa kusimamia serikali ilipoonekana kwenda kombo .Hata haki na mamlaka ya bunge yalipoingiliwa wabunge walibaki na vyama vyao .
Leo hii ninapo tafakari, nini umuhimu wa waheshimiwa wabunge kuwepo katika bunge,iwapo kazi zao zinaweza kufanyika na watu wachache tu?Ninaona ipo haja ya kulivunja bunge hili na kuokoa fedha za taifa zinazotumika kuendesha vikao vya Bunge.