Hapa nimeoenda mumbe hawa wanaotuambia huku mtaani ni lazima wanatoa wapi huo msemo
Hilo neno "lazima" ni la kisiasa, lakini ukweli kisheria mafunzo ya mgambo ni ya hiyari.
Ngoja nikwambie inavyofanyika:
Kinapofika kipindi cha mafunzo hayo, mshauri wa jeshi la akiba ambaye ni mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, hulipeleka jambo hilo kwenye meza ya mwenyekiti ambaye ni DC.
Likiishakupata baraka, basi huyo mshauri hutafuta wagambo waliomaliza mafunzo ya uongozi wa Mgambo ili kusaidia kufundisha wanafunzi wanamgambo wapya.
Hao wakufunzi wanamgambo hufundisha kwa kujitolea na malipo ya posho zao ni faini mbali mbali zinazotozwa kwa watoro wa kila siku na wanaostahili (registered)lakini wakakaidi mafunzo.
Kipindi hicho cha mafunzo, kuna kauli kama hizo za mafunzo ni "lazima" ili ukijichanganya utozwe kwa ajili ya wakufunzi.
Kifupi jambo hilo ni hiyari, na kama hautaki kushiriki, sema wazi hata bila kisingizio kuwa "sipo tayari kushiriki", uone kama watakupeleka popote.
Kama kutakuwa na ubabaishaji zaidi, waambie wakuoneshe maandishi yanayohusu sera za mgambo ni wapi ilipoandikwa "mafunzo ya ngambo ni ya lazima"? Hakuna, bali imeelezwa wazi kuwa mafunzo hayo ni ya hiyari na kama kuna faini yoyote ya kibabe, pambana na ukatae kutoa.
Wakikuona una mwamko, watakuvutia nyuma ya jengo ili "usimwage mtama kwenye kuku wengi" na kukufukuza uende zako!