UMMY MWALIMU -UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA UENDE SAMBAMBA NA USALAMA WA CHAKULA

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
389
272
UMMY MWALIMU -UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA UENDE SAMBAMBA NA USALAMA WA CHAKULA

Katika kuadhimisha Siku ya wanawake Duniani 2017, leo Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) ameungana na wanawake wa Mkoa wa Singida, katika
aa8aafb78fb4ad23330d5a36ebe874aa.jpg
Manispaa ya Singida. Akiwa katika shughuli za maadhimisho hayo mkoani Singida Waziri Ummy ametembelea mradi wa Wanawake wa IR VICOBQ Ititi Singida ambao ni wa kuzalisha viazi lishe.

Akiwa katika Mradi huo wa wanawake wa kuongeza thamani ya mazao, Mhe Ummy amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa (UN Women) kwa kuwekeza katika shughuli za wanawake ambao ndio wazalishaji wakubwa wa Chakula na bidhaa za viwandani.

Mhe Ummy ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaongeza jitihada ktk kuwapatia fursa na mikopo ili waweze kushiriki kikamilifu ktk uzalishaji wa bidhaa za viwandani na bidhaa za chakula.
 
Back
Top Bottom