Ummy Mwalimu aitaka bodi ya NHIF kuandaa utaratibu wa mpito kuhusu Bima ya Afya kwa Jamii

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
36,076
29,633
Kwa wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka moja ya jambo lililoahidiwa na Magufuli kupitia Ilani ya CCM ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaunganishwa na mifuko au mfuko wa bima ya Afya.hili alilisisitiza sana katika kampeni zake hasa hasa siku za kati kati na mwisho wa kampeni.

Ni bahati mbaya watanzania wengi sio wafuatiliaji na wadadisi kwa kile kinachozungumzwa na wanasiasa wakati wa kampeni na badala yake tunabaki kushindana kwa kuzungusha mikono au kukata viuno.

Ikumbukwe pia wakati wa mjadala wa wagombea urais ulioandaliwa na TWAWEZA ambao ulirushwa live kupitia JF ...mimi niliuliza swali kuhusu msimamo wa wagombea urais juu ya jamii kujiunga na mifuko ya afya ya jamii...swali hili lililenga kujua msimamo wao kuhusu swala hili kwamba liwe la lazima au hiari...

Kwa bahati mbaya hakukuwa na mgombea yeyote aliyeweza kurespond kwenye swali hili.

Tukijikita kwenye mada ...

Nimefurahishwa na dhamira ya Ukweli ya Mh Rais...yaani kutenda na kufanyia kazi yale aliyoyaahidi ndani ya muda mfupi tena kabla hata ya kuanza kutumia bajeti iliyopangwa na serikali yake.

Waziri wa Afya ndugu Ummy Mwalimu amesikika akiitaka bodi mpya ya NHIF chini ya Mama Makinda kuhakikisha inaratibu smooth transition ya kubadilisha mifumo iliyopo ya Bima za afya kuelekea mfumo mmoja wa bima za afya kwa wote.

Hili sio jambo dogo au la mzaha .
.ni jambo muhimu na liliwahi kuleta msuguano katika nchi ya marekani.

Hivyo tuimbee bodi mpya ya NHIF iweze kulisimamia hili na kuliwekea utaratibu utakaofanya wenye nacho na wasio nacho wanafaidika.
 
Bima ya afya iwe lazima kawa kila mwananchi. Lazima hii itafutiwe miundombinu ya kuwa lazima.
Hili ndio kimbilio la uboreshaji wa huduma kwenye sekta ya afya ...hapa itapelekea vituo vya huduma kushindana ili kuweza kuvutia wateja.
 
Kuna implementers ambao wameboresha sana mfuko wa jamii-CHF kuwa insuarance. Kuna mradi upo Dodoma unaitwa Health Promotion and System Strengthening -HPSS-Project wako funded na serikali ya Swiss. Wametengeza mfumo mzuri sana ambapo kwa sasa kila kaya inakua na kadi yake ya CHF na wanapata matibabu kuanzia ngazi ya dispensary hadi hospitali ya mkoa. Kaya yenye watu 6 inachangia 10,000TSH na wanapata matibabu mwaka mzima. HPSS wametengeneza mfumo wa IT unaosaidia shughuli zote za Insuarance unaoitwa IMIS-Insuarance Management Information System. Ni mfumo mzuri sana na kwa sasa unatumika cameroon na Nepal na pia wakenya wameshaomba kuuchukua wautumie. Kwa sasa hiyo CHF iliyoboreshwa inafanya kwenye mikoa ya Dodoma,Morogoro na Shinyanga chini ya HPSS na wateja wanapata huduma kwenye mkoa wowote kati ya hiyo sababu ya kutumia huo mfumo wa IT ambao huwatambua wateja popote pale.
Ni oportunity kwa NHIF kutumia hiyo system na wakiweza kwa kusaidiana na wadau wasambaze nchi nzima huo mfumo.
CHF ni mkombozi wa afya hapa nchini.
 
kwa nini tuwe na mjadala kwa miaka 5 juu ya bima ya afya kwa wote??Tufikie mwisho
 
Back
Top Bottom