Kama baba angekuwa baba bora kwa watoto wake na mume mzuri kwa mke wake, mama angekuwa mama bora kwa watoto na mke bora kwa mume wake.
Watoto wangeangalia wazazi na kutamani nao kuishi na kuwa na wenzi wao. Dysfunctional families imekuwa chanzo cha matatizo mengi sana, watoto kuingia katika makundi ya ajabu, wazazi kuchelewa kujua kuwa mtoto keshaharibika.
Mzazi anasoma kwa gazeti kuhusu mtoto wake, hii ni ishara ya kukosekana kwa mawasiliano mazuri katika familia, maana hata kama mzazi angekuwa kapitiwa ndugu zake huyo mtoto wanakuwa wapi? Ujenzi wa Taifa bora unaanzia katika ujenzi wa familia.
Ukishaharibu kwenye familia Taifa linabomoka. Moja ya mambo yanayotokea siku hizi watoto kujiunga magroup hatarishi watu wanajiuliza huyu mtoto ana kila kitu nyumbani, wanasahau kujiuliza je nyumbani kuna upendo, kuna amani, kuna mawasiliano.
Wewe endelea kutokumjali na kumheshimu mzazi mwenzio, kujibizana na makelele mbele ya watoto, kutokujali hisia za watoto, unawapa hela unaamini hayo ndio majukumu yako kama mzazi, unaact kama sponsor na sio mzazi, hauna chochote watoto wako wanachojivunia isipokuwa fedha yaani wakikumbuka baba au mama hasira inawaajia jinsi ambavyo kutwa wewe ni kelele au dharau kwa mzazi mwenzako,
Hauna muda nao na wala hujui ni mangapi wanapitia. Single mother/father naye anaweza lea vizuri kwa kuepuka kupanda mbegu za chuki kwa watoto na kuwa na muda na watoto. Kuna ya kulaumu serikali ila mengine ni sisi wenyewe wazazi tunatengeneza majumbani kwetu.
"Money and Fame are not everything"