Umeme wa TANESCO usivoisha kukatika

mutanim

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
203
77
Naishi Kigamboni, kwa siku kadhaa ambazo nimekuwapo nyumbani kipindi hiki cha mwisho wa mwaka, nimeshuhudia umeme ukikatika si chini ya mara kumi kwa siku. Mara nyingine unarudi baada ya kati ya dakika kumi mpaka nusu saa, muda mwingine unarudi baada ya lisaa na kupokewa na wananchi kwa shangwe wote mnazifahamu.

Umeme ukikatika, wazo linalofuata kama ni muda wa giza, utasikia kuulizana, "mshumaa, taa ya kichina au vibatari", Yaani tumeshazoea na tunachukua hatua mbadala haraka na kuendelea kuusubiri, bila habari utarudi saa ngapi?na labda ni sababu gani inafanya huko kurejea rejea kukatika kwa hii nishati muhimu,

Mimi kama mhandisi na raia mwenye maslahi, nafikiria kwamba ndugu zetu hawa hawaitendei haki jamii na taaluma yao kabisa.

Nikwambie kitu, Financial experts huwa wanaweza kuwaaminisha wawekezaji kwamba watapata faida kiasi fulani wakati wa makisio (budgeting/projections/ forecast), na waungwana wakaninua kwa wingi shares zao, lakini mwisho wa siku, wanaruhusiwa kuja na actual results kinyume na matarajio huku wakitaja sababu kama oooh, mfumuko wa bei, hali ya kisiasa, hali ya kiuchumi katiaka soko la dunia n.k, na hakuna sheria strict inayoweza kuwawajibisha mara moja, mpaka labda hatua za makusudi ambazo inatokea nchi nyingine,

Lakini kwa wahandisi, hakuna hiyo nafasi, unao uwezo wa kupanga (plan effectively), na actually ku predict the outcome kwani inputs zote utakuwa unazo wakati wa kufanya m radi (project planning),

Labda nisiende mbali sana, ila tu niwaulize, je wanayo shida gani honestly ambayo inawazuia kusema ukweli wa uwezo wao kwa sasa? wakiwa wawazi(transparent) watapunguza mno lawama. La, watu watakuwa na maelezo yasiyo rasmi kila mara na kumalizia kushusha imani ya wateja wao.

Kwa kweli tunahitaji kuanzisha hashtag ya #utilityconsumersrights ili haki za walaji ziheshimiwe.
Umenunua umeme, bandle za wenye simu, umelipia maji au DSTV post payment n.k and yet unakosa huduma as if it was nothing, hakuna hata matamko kuonyesha kwamba nao haya yanawakera.
 
Tanesco bila kusikia wamefukuzwa wafanyakazi 200 na bodi kuvunjwa matatizo ayatakwisha .nimeota hivyo .
 
Back
Top Bottom