SPACED
Senior Member
- Jun 7, 2016
- 137
- 132
Katika uchaguzi uliopita tumeshuhudia ukitawaliwa na figisufigisu nyingi za kuukwaa ukubwa ndani ya vyama nje ya vyama(jimbo). Demokrasia iliwekwa pembeni, wapo waliojinasibu kwa uchungu mkubwa kubeba hisia na unyonge wa wapiga kura kwamba wao ndio wanajua vizuri namna ya kupambana na serikali inayowaumiza, wakaonewa huruma wakaaminiwa na kuchaguliwa.
Sasa siku zinahesabika za Naibu Spika ambae kwa muda mrefu ameliongoza bunge hili kuwarejesha wakubwa hawa makwao, kila mbunge kwa sasa anapanga karata zake vizuri na gia atakayokuja nayo huku mtaani. Alichojigamba akiwa jukwaa la kutafutia kura na alichokichangia bungeni kama vina uhusiano na maisha ya makapuku huku mtaani.
Najua wapo wanajua kabisa kuwa wanasubiri kupewa makavu live majimboni hasa yule mbunge wangu aliyedondosha machozi jukwaani akidai anaguswa sana na maisha yetu ingawa hakuwa chaguo letu tukamwonea huruma kwa sharti arudi jimboni mara tu vikao vyao vinapoisha, akakubali. Tunausubiri mrejesho huku kamati zinazoandaa mahojiano na ww ziko hatua za mwisho kadri muda wako unavyoelekea mwishoni.