Nakushauri mwache asome Loyola High School na wala usijali kabisa kumwamishia huko Umbwe. Kwanini
1/Loyola ni miongoni mwa Private catholic day school zinazofanya vizuri sana hapa Tanzania kielimu. Ninaijua shule hii vizuri sana toka mwaka 1995 wakati inaanzishwa. Suala la kufaulu ni lazima na suala la kufeli halipo kabisa.
2/Loyola High School wana uhakika wa walimu wa kutosha na mazingira mazuri sana ya kielimu huenda kuliko shule nyingi sana.
3/Loyola High School wanaushindani mkubwa sana wa kusoma miongoni mwa wanafunzi, kuna kitu kinaitwa Cut off point kutoka kidato kimoja kwenda kingine.
NOTE
*Kufaulu kwa mwanafunzi kunategemea vitu vingi sana ikiwemo JUHUDI BINAFSI.
*Shule za serikali hazina tofauti sana kimatatizo. Mfano Chakula kibovu, Magonjwa ya mlipuko, Ukosefu wa walimu, ufuatiliaji duni wa kitaaluma.
*Ufaulu katika shule za serikali ni jambo lisiloweza kutabirika, trend zao hazieleweki kabisa.
*Shule za Private nyingi(Kama Loyola) ni gharama sana.