Umakini unahitajika uchaguzi BAVICHA

Umakini unahitajika uchaguzi BAVICHA

Joined
Oct 21, 2010
Posts
39
Reaction score
34
Kwa wenye mapenzi mema na CHADEMA, kwa kuwa baraza hili la vijana lina vijana wengi wenye uwezo, waaminifu na wapenda maendeleo na wamekubali kujiunga na jeshi hili la ukombozi wa pili wa Taifa letu,uchaguzi huu unaondelea ni matumaini yangu kuwa watajitokeza wengi tangu ngazi za chini za uongozi hadi juu, ili kupata viongozi imara wa baraza watakaoakisi taswira ya BAVICHA ndani na nje ya nchi.

Na pia wanahitajika viongozi wasikuwa na historia ya usaliti, ruswa, ugeugeu na wasioweza kutumiwa na maadui wa ukombozi wa nchi yetu.ni muhimu viongozi hawa pia wakipimwa kwa uadilifu na utiifu wao katika chama na taifa kwa ujumla,uwelewa wa misingi, falsafa na itikadi ya chadema.

Zaidi ni lazima wapatikane viongozi wakaosimamia baraza la vijana kwa kuandaa kisaikolojia vijana wezao na kuwaunganisha kwa maandalizi ya kuchukua dola katika uchaguzi ujao. Watakaoshinda wasiwabeze wenzao na watakaoshindwa wasilikimbilie msituni kuhujumu walioshinda.
Hatutegemei kuona hujuma, matusi, kudhalilishana na ruswa katika uchaguzi Bavicha, kwani hili ndilo Baraza pekee linalobeba matumaini ya vijana hapa nchini.

NI WAKATI WA CHADEMA KUWA MAKINI ZAIDI.
 
Chadema haiwezi toa viongozi bora labda waliyo Asi ccm Kama akina Slaa shibuda waitara banyanga nk wengi wanywa viroba tuu
 
Back
Top Bottom