Yesu hakufa ili watu wamiliki majumba na magari.
Injili yoyote ile itakayohubiriwa hapa duniani au popote pale kama haimwongozi mtu kuacha dhambi na kumfundisha pamoja na kumwombea muamini ajazwe Roho mtakatifu na badala yake kutia kelele kwenye maspika kuwa mara ooohh utainuliwa!, utatajirika!, utajenga! n.k hiyo ni Injili ya kishetani na muhubiri jehanamu inamngoja
Kuna wahubiri wa kishetani wanaotumiwa na shetani kwa namna mbili;
1.Kwa kujua
2.Kwa kutokujua.
Ukikaa vizuri na Mungu kila kitu kitakuja automatically, hapa simaanishi kuwa ni lazima uwe tajiri.