Ulishawahi msaidia mtu/watu ambao leo hii wameshakutelekeza baada ya kuanguka?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Kuna jamaa wangu alikuwa ananiadisia kipindi ana ajira nzuli alikuwa ana moyo wa kusaidia ndugu jamaa na marafiki pale wanapomueleza matatizo wanayopitiaaa. .....

Leo hii baada ya mktaba wa kazi kuisha na kupoteza ajira aliyokuwa nayo wale watu ambao alikuwa anawasaidia kipindi wana shida karibia wote wamemkimbiaa.

Mbaya zaidi hata watu aliokuwa nao karibu wengine hawapokei simu zake na wengine wametelekeza licha ya mshikaji kwa sasa anapitia katika hali ngumu kuanzia yeye na pamoja na familia yake????

Je upande wako ww ulishawahi kuwasaidia watu au mtu wakati una uwezo na leo hii wamekutelekezaa baada ya kuangukaa.
 
Ila sijaanguka , nimejikwaa tu ha ha ha ha ha ha....
Niliowasaidia ni Wengi tu, Ila siwalaumu ksb huwenda wana sababu ya msingi yakutotaka kuwasiliana na Mimi kwa namna yoyote ile.
Yote nimemwachia Mungu ksb Mimi siyo mkamilifu, hivyo sipashwi kuwahukumu kwa namna yoyote ile , pia kila jambo na wakati wake.
 
Huo huwa ni upumbavu wa kupindukia, unasaidia ukitegemea uliemsaidia aje akusaidie! Ukiwa na nafasi ya kumsaidia mtu msaidie ondoka.
 
mi ndo inanitokea sasa, kuna jamaa nilimuunga na mshua flani akampa shavu la uhasibu kampuni flani. now sina mchongo nimemcheki aniunge na kampuni rafiki na yao jamaa ananikwepa.

ila haina noma, najua hana mbio kwenye mchanga ngoja nikomae na mambo yangu tu.
 
Unapo saidia mtu hata kama ni mtoto wako wa kuzaa usitegemee asilimia 100 siku moja hatakuja kulipia wema wako wa awali.
Duniani kila mtu ni mmoja mmoja si habari ya kufanana vinasaba wala udugu duniani ni mtu mmoja mmoja ktk nafsi moja tu.
Hapo ndo msemo wa tenda wema nenda zako uchukua nafasi.
 
hiyo ipo sana mkuu watu wanatofautiana hata mi kuna dogo mmoja nilimtoa bush nikamuweka kwenye kaofisi changu cha kuchezesha video game, akafahamiana na watu na baadae akapata shavu akaenda dubai kufanya kazi huko...

Cha ajabu hata nikimcheki kupitia fb kumsalimia tu anajifanya kama msg zangu hazioni, nikaamua kumpa hi kupitia comment za picha zake anazo upload cha ajabu ikawa kama hazifatilizi... basi nikampotezea tu..

Watu hubadilika!
 
Mimi kuna ndugu yangu huyo niliwahi kumsaidia kwa kumpaga ""cheti changu cha form four

Apate ajira tasisi flani hivi ya watu binafsi sasa baada ya kupata kazi hata siku moja tangu aanze kufanya kazi hakuwahi kunishukuru wala kusema hata kunipa hela ya vocha hakuwai,

Sasa majuzi juzi ile kampuni aliyokuwa anafanyia kazi imefugwa na mktaba umeishaaa na kazi saivi hana yupo kitaa tuu basi tangu apoteze ajira yake ndio naona ananikumbuka mara anakuja kunisalimia

Basi mi namwangalia wee nashidwa tuu kummalizaa
 
Achilia mbali jamaa na marafiki, ndugu zako wa damu unawasaidia leo lakini wanakuchukia hatari. Siku ukikwama sio tu kwamba hawakusaidii, wanakusema vibaya na kusahau yote uliyowafanyia.

Watendee mema watu kadri upatapo nafasi, mambo mengine mwachie Mungu.
 
Wasengerema hao kudadek
Hyo ishanitokea 2015

Na ndo nlikoma kumsaidia
Rafik hata awe wa ukarbu gani
 
Unapo saidia mtu hata kama ni mtoto wako wa kuzaa usitegemee asilimia 100 siku moja hatakuja kulipia wema wako wa awali.
Duniani kila mtu ni mmoja mmoja si habari ya kufanana vinasaba wala udugu duniani ni mtu mmoja mmoja ktk nafsi moja tu.
Hapo ndo msemo wa tenda wema nenda zako uchukua nafasi.


Wahenga walinena

Hawa wahenga nina uhakika ni watu walikua na uwezo/elimu na maarifa makubwa mno. Waliyoyasema yanatokea

Ila ukimsaidia mtu we potezea. Kuna wengine unakuta ulimpiga jeki sehemu fulani ndo hadi anaanza kukukwepa akidhani ni deni. Msaada ni msaada na haulipiki na kama ni deni au mkopo hapo nafuu ukinikwepa ntaelewa. Ila sio kwa tendo la wema "MSAADA"
 
Back
Top Bottom