Ulishawahi kupishana na gari la mshahara?

Ulishawahi kupishana na gari la mshahara?

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,729
Jamaa yangu kapigiwa simu mara nne na namba ngeni hakutaka kupokea. Yeye alijua ni jamaa anayemdai akaona auchune, maana atamjibu nini? Pesa yakumpa hana, vyuma vimebana hadi vinaingia kutu, hata grisi imegoma kulainisha!!

Baadae akaona embu ahakikishe jina kwa kujaribu kufanya kama anatuma pesa maana jina huwa linatokea. Alipofahamu namba ni ya wapi/nani akaona aipige.

Kupokelewa kumbe ilikuwa ni namba toka kwa moja ya bahati nasibu zinazochezwa hapa nchini na namba yake ilishinda 10M.

Hadi sasa utafikiri kafiwa kwa mshtuko aliopata na majonzi aliyonayo!!!

FUNDISHO:-
Mdeni haui, anadai tu, naye ni binadamu, usimkimbie kwa kuzima simu au kutopokea simu, utampa hasira zaidi na pia mambo muhimu yatakupita.
Ongea naye tu kiungwana!
 
Back
Top Bottom