Ulipaji wa kodi/TRA

Ulipaji wa kodi/TRA

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,508
Reaction score
13,974
Heshima kwenu wote.
Nimekuwa nikisafiri mikoa mbalimbali ndani ya Tanzania.
Nimeshuhudia baadhi ya wafanyabiashara hawatoi risiti za EFD.
Katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro maeneo mengi wanatoa risiti kutokana na malipo yaliyofanyika.(Hutoa bila kuombwa)
Lakini maeneo mengi Tanga mjini hawatoi risiti kabisa kwa mfano mgahawa wa Kibarua uliopo karibu na stendi ya mabasi ya Zamani(barabara ya 12)
Pia kwenye maduka ya vifaa vya ujenzi nimetembelea Saifi store,jirani na mahakama ya Mwanzo/Wilaya ya Tanga,nao hawatoi risiti za EFD zaidi wanaandika risiti za mkono.
Nilichojifunza hawa wafanyabiashara wenye asili ya Kihindi na Waarabu hawana hofu wala kujali kuhusu kutoa risiti za EFD na hata ukiwauliza wanakuambia kama hutaki kununua ondoka.
Nauliza hivi TRA nchi hii ziko ngapi? Au kuna watu/maeneo hawaruhusiwi kulipa Kodi kupitia mauzo?
Angalizo:Kuna baadhi ya wafanyabiashara waaminifu Tanga mjini hutoa risiti kwa kila mauzo kwa mfano Central bakery nk

Kazi kwenu!!
 
Ingia kwenye biashara siku moja wakutandike hizo kodi utajua kwa nini hawatoi risiti.Hizo kodi zingekuwa fair kungekuwa hakuna ukwepaji na risiti zingetoka bila kuomba.
 
Back
Top Bottom