Ulianzaje Kushabikia Timu unayoipenda ..Mimi nilianza hivi..!

King_Villa

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
575
378
Nakumbuka mwaka 1998 France wanachukua kombe la dunia Niko darasa la tatu Mdogo sana ila nafuatilia mpira hatari !
Nakumbuka Kwenye fainali hiyo hiyo zinedine zidane (zizou) anafunga goli Kali sana Lililosababbisha Mimi na watoto wenzangu kushangilia mpaka tukadondosha TV ...
Nilichezea kichapo kikali sana mpaka nilivimba miguu!
Haikuishia hapo siku iliyofuata nilichukua koti langu la shule nikaliandika mgongoni zinedine zidane ..
muda wa darasani Mwalimu wa zamu akaniona nimelivaa hilo koti asee alinimind akanipeleka offisin kwake huko offisin kumejaa walimu kama sita ..nikapitishwa Kwa kila Mwalimu nikala viboko vitatu Kwa kila Mmoja !
Haikuishia hapo nilipelekwa mbele ya shule nikala viboko kama saba viliuma sanaaa..
Huo ulikuwa mwanzo wa kuipenda ufaransa hadi Leo ndio timu Yangu ninayoikubali dunian hata ifungwe ngapi mi ni ufaransa?

Sijui wengine mlianzaje kushabikia YANGA na Simba
 
Mkuu kwani wewe ni mtanzania au mfaransa?
(uzalendo kwanza)
 
Tim zang zote zmeniangusha
Zmeshuka kiwango co kawaida

Italy, Netherlands
 
Kijijini wakati huo nahitimu ly nilifungua kijiwe cha kubrashi viatu...nikaenda Kwa fundi kuchomelea nikaokota kopo la rangi nyekundu ya geti iliyobaki...ikatumika kuandikia jina na kijiwe changu... MANCHESTER SHOE SHINE...nikachora na buti kuubwaaa...rangi maarufu wakati huo za viatu zilikuwa
White
Dark tarn
Nyekundu
Na black

Nyekundu wateja wangu wakubwa walikuwa walimu
White wateja Wana kijiweni
Petroli pia wana
Black walokole...hawa viatu walikuwa wanaleta jmosi

Tulikuwa na draft na vijiwe enzi zetu vilikuwa vinajaza kinoma hapo draft pale solo...waongo wanatuuzia chai (maneno ya uongouongo) basi Kwa vile kijiwe kilivyokuwa maarufu Kwa jina la man u ikawa ndo hadi kesho mani chama langu...Man U wote gongeni like hapa Kwa mwana.

That was 1997
 
kipindi hicho hata sijui timu za bongo, ba mdogo alikuwa anaupiga mwigi sana basi alikuwa ananichukua kwenda kwenye soka.

akawa ananambia mi yanga, huku home mzee ni simba damu damu ana kadi, kofia imeandikwa simba taifa kubwa (mpaka leo ipo ) na simba ikishinda anakwambia njoo mle matunda ya simba (ananunua vinywaji na linapikwa pilau)

familia nzima wako simba mi ndo nilikengeuka kutokana na kuambatana na ba mdg, hii imepelekea upinzani na mzee hasa hii miaka 3 nyuma.

simba akifungwa mzee ananyong'onyea kama mgonjwa, leo wako nafasi nzuri anatamba balaaa mpaka napata moto kwa nini yanga wamezingua ivi.

mpaka kesho mi yanga sana.
 
Mwaka 2012 brother angu alinichukua kwenda taifa kucheki simba na yanga... zile gonga na snake pass za simba siwezi kuzisahau!! Siku hiyo yanga alidundwa 5 kwa yai.. yaani hadi kipa wa simba (simkumbuki jina) siku hiyo alitupia... basi tangu siku hiyo mi ukinitajia yanga nakuona hamnazo tu hujielewi!!
 
Mwaka 1999 wakati wa kipindi cha chemsha bongo ya redio one stereo liliulizwa swali, "klabu ipi imetwaa ubingwa wa ulaya". Jibu likawa Manchester United. Kuanzia hapo nikawa shabiki wa united mpaka kesho
 
Mie nilianza kuipenda simba sijui ilikua 2003 vile, pale ilipokua moto wa kuotea mbali, nakumbuka pale ilioowatoa zamaleck, ili nivutia pale walipocheza nje, vile wazungu, walikua wanaitaja yani simba sports daresalaam, kwa rafudhi ya kizungu, hapo ndo ulipoanzia ushabiki wa simba, nakumbuka pia tuliwatandika inyimba fc ya Nigeria goli mbili kwa 0 wakati huo Nigeria iko hot, enzi za akina okocha, nakumbuka tulivyokwenda Kwao baba, halalaaalah, walitutungua 4 kwa 0.
 
Mimi kila mwaka wa World cup huwa nachagua timu 2006 nilichagua Ufaransa 2010 nikachagua spain 2014 nilichagua Ujerumani. 2018 niko argentina

Club ya arsenal aliyefanya niishabikie ni mnyama fulani anaitwa Fredriu Ljungberg yaan huyu jamaa alipiga bao mechi ya nusu fainali kombe la FA dhid ya bolton tukashinda 2-0 Roberto Pires alinifanya niamini hakuna kama arsenal duniani jaman kwa anayeijua ile arsenal mi siendelei kusema hapo nipo darasa la kwanza

Simba na Yanga nilikuwa simba kwa kuwa mjombangu alikuwa simba ila nilipokuwa kidogo nikiwa la 6 nilijitambua na kujua moyo wangu upo kwa yanga maana hata simba na yanga zikicheza simba akishinda nilikuwa nashindwa kushangilia nahis tumebahatisha,

Hii imenifanya nisioe kwa mkumbo kisa wenzangu wanasifia chura basi nioe mwenye chura hapana nasikilza zaid sauti ya ndani.

Na sijutii na mnajua Yanga ni mume halali wa simba.
 
Mwaka 2010 brother angu alinichukua kwenda taifa kucheki simba na yanga... zile gonga na snake pass za simba siwezi kuzisahau!! Siku hiyo yanga alidundwa 5 kwa yai.. yaani hadi kipa wa simba (simkumbuki jina) siku hiyo alitupia... basi tangu siku hiyo mi ukinitajia yanga nakuona hamnazo tu hujielewi!!
Huna hata kumbukumbu vizuri 2010?????
 
Mie nilianza kuipenda simba sijui ilikua 2003 vile, pale ilipokua moto wa kuotea mbali, nakumbuka pale ilioowatoa zamaleck, ili nivutia pale walipocheza nje, vile wazungu, walikua wanaitaja yani simba sports daresalaam, kwa rafudhi ya kizungu, hapo ndo ulipoanzia ushabiki wa simba, nakumbuka pia tuliwatandika inyimba fc ya Nigeria goli mbili kwa 0 wakati huo Nigeria iko hot, enzi za akina okocha, nakumbuka tulivyokwenda Kwao baba, halalaaalah, walitutungua 4 kwa 0.
Doh!
 
Daaaaah mi kwa Bongo nimeanza nimeanza kuipenda simba enzi za akina pawasa, Selemani matola 2003 ka sikosei. Ulaya Barcelona_ kipindi cha fainali ya UCL 2006 zidi ya Arsenal Spirit waliokua nayo Barcelona na mpira waliokua wameupiga kipindi cha pili . Toka hapo hata Barcelona asichukue chochote au afungwe bdo mi Barcelona. Ila nashkru Tangu nimeanza kuipenda Barca haijaniangusha.
Ukija Timu ya Taifa ni Brazil hapo ilikua 2002 kule japani game zinachezwa saa mbili asubuhi Achana Ronaldo De Lima.
 
Kwa bongo nilianza kuipenda yanga baada ya bro yeye kuipenda simba (huwa napenda upinzani by nature). Na epl kipindi cha miaka ya 2000 kulikuwa na timu mbili ambazo zilikuwa zinasifika sana. Man u na arsenal. kwa kipindi kile man u ilikuwa na wachezaji weupe tu (sina uhakika kama walikuwa na black hata mmoja). So kwa kuwa arsenal walikuwa na weusi kadhaa nikaona ndo timu nzuri haina ubaguzi. Hence arsenal mpaka kesho. Hata ifungwe vipi
 
Back
Top Bottom