VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Tangu kupigwa marufuku kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa mwaka jana, idadi ya wanasiasa wanaokamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya 'uchochezi' imeongezeka. Kinara wa wanasiasa waliokamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi ni Mbunge Tundu Lissu wa Singida Mashariki (CHADEMA).
Mwingine aliyekumbwa na kadhia ya 'uchochezi' ni Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema. Hadi muda huu, Lema yuko mahabusu katika Gereza la Kisongo baada ya dhamana yake kukwama. Ikaripotiwa pia kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Maendeleo) Zitto Kabwe naye anasakwa na Polisi. Wazushi wakazusha kuwa ametoroka hadi nchi!
Pia, kuna wimbi la viongozi wa kisiasa kuhukumiwa jela baada ya katazo hili la mikutano ya kisiasa. Kuanzia kwa Mbunge Lijualikali (Kilombero-CHADEMA); viongozi wa CHADEMA kule Mtwara; viongozi wa CHADEMA kule Mara na kadhalika, ni mwendo wa mahakama na hukumu zake. Ni mwendo wa hukumu za 'hakimu'.
Naamini, hata kama sitaungwa mkono, kuwa kupigwa marufuku kwa mikutano ya hadhara ya kisiasa nchini Tanzania kumechangia kuongezeka kwa 'wachochezi' na 'uchochezi' kwa ujumla. Wanasiasa wamekosa pa kusemea na kuikosoa Serikali. Wanajikuta wakinaswa facebook na twitter au hata simuni kwa 'kuchochea' wananchi.
Halafu, kwanini wachochezi wawe wapinzani tu? Kaswali ka kizushi: Lissu ameshafikishwa huko Dar es Salaam baada ya kukamatwa Dodoma?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini Singida)