Ukweli Ujulikane

Ukweli Ujulikane

isotope

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
2,392
Reaction score
817
Hii sala inasaliwa nchi nzima kila siku na hasa hasa jumapili (na takribani watu milioni ishirini). Ukweli utajulikana!
SALA YA KUMUOMBA MUNGU AWAFICHUE WANAOPANGA MAOVU DHIDI YA WAKRISTO (NA RAIA WEMA WENGINE)
Bwana Yesu, Mfalme na Kiongozi wetu, uwe nasi katika safari yetu ya Imani. Sisi tunaosadiki, tunaamini katika ahadi zako. Wewe ulisema: “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwamini Mungu niaminini nami pia……Anayeniamini atafanya mambo makubwa ninayoyafanya mimi, naam atafanya hata makuu zaidi…..Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya”(Yn 14:1,12,13).
Tunakuomba uwafichue wale wote wanaopanga na kutekeleza uovu, ili kufikia malengo yao yasiyo na tija. Ukweli ujulikane. Ee Bwana, inuka ujitetee. Usikifedheheshe kiti cha Ufalme wako. Waliokuinukia walegee. Nasi kondoo wako ututunze. Kama mboni ya jicho lako utulinde. Ee Mungu wa Amani utusikie. Nasi tutalisifu jina lako milele. Amina.
 
Baba uliye mbingu tunakuomba uikubali sala hii. Amen! Amen! Amen!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mshaaanza chokochoko!
Kila mtu akae na imani yake hakuna ajuae ukweli!
 
Kujua tatizo ni sawa na kupata nusu ya suluhu yake.

Kwa hiyo unatafuta suluhu???
Kwa hili huwezi pata....!! kwani imani zinatofautiana saana na kila mtu anajiona yeye ni zaidi ya wengine.
In short ur wasting ur time on this.
 
Hizi bunduki za wapi jamani? Naskia milio ya risasi huko Manzese
 
Kwa hiyo unatafuta suluhu???
Kwa hili huwezi pata....!! kwani imani zinatofautiana saana na kila mtu anajiona yeye ni zaidi ya wengine.
In short ur wasting ur time on this.
Mbona unaonekana kukwazika na hili, limekugusa? Au ndo miongoni mwa wanaopanga na kutekeleza huo uovu? Kama umeona njia hii siyo effective pendekeza ya kwako, ili suluhisho lipatiakane.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom