Ukweli tupu; Hadi sasa sijajuta kumpa kura Lowassa

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,182
2,015
Naanza kuamini kuwa nilikuwa sahihi zaidi kumpatia kura yangu ndugu Edward Lowassa.

Kwa hali ya sasa kule Zanzibar, mgogoro wa umeya Dar na Tanga, uamuzi wa "mr. Wakukurupuka" wa kuwatimua watumishi wa umma bila hata kuwasikiliza, uminyaji wa demokrasia na kuminya vyombo vya habari inanipa shaka sana.

Ndani ya siku 100 tu mtani wangu Ngosha kafanya makosa mengi sana, tena yasiyo ya msingi. Japo kafanya mema pia ila yamefunikwa na mabaya kwa kuwa yamekuwa kero kubwa.

Janja janja ya bongo movie ya kuongea mbele ya kamera za TBC, STAR TV, CLOUDS na mic za UHURU na TBC-TAIFA hauwezi kutufumba macho tunaotazama mwendo wa kuvizia na kutunisha misuli wa serikali.

Ndo maana hadi leo sijawahi kujuta ile october 25 kura yangu kumpa laigwanan.
 
Naanza kuamini kuwa nilikuwa sahihi zaidi kumpatia kura yangu ndugu Edward Lowassa.

Kwa hali ya sasa kule Zanzibar, mgogoro wa umeya Dar na Tanga, uamuzi wa "mr. Wakukurupuka" wa kuwatimua watumishi wa umma bila hata kuwasikiliza, uminyaji wa demokrasia na kuminya vyombo vya habari inanipa shaka sana.

Ndani ya siku 100 tu mtani wangu Ngosha kafanya makosa mengi sana, tena yasiyo ya msingi. Japo kafanya mema pia ila yamefunikwa na mabaya kwa kuwa yamekuwa kero kubwa.

Janja janja ya bongo movie ya kuongea mbele ya kamera za TBC, STAR TV, CLOUDS na mic za UHURU na TBC-TAIFA hauwezi kutufumba macho tunaotazama mwendo wa kuvizia na kutunisha misuli wa serikali.

Ndo maana hadi leo sijawahi kujuta ile october 25 kura yangu kumpa laigwanan.
HUNA AKILI
 
Politically, Lowassa is finished!

Hata wafuasi wa shetani watakuambia uamuzi wao kumfuata shetani ni bora kuliko kumfuata Mwenyezi Mungu! Hii haina maana walichokifanya kina manufaa katika maisha yao yajayo!

Ujinga ni mzigo!
 
Haya ni mawazo huru! Tujifunze uungwana kwa kusikiliza watu wote hata wale ambao hatujaendananao kimtazamo, binafsi sioni sababu ya kumtukana mtoa mada! Hayo anayoyasema ni mawazo yake huru, kumuita kuwa hana hakili ni kukosa akili zaidi, je ulitaka awe na mawazo yanayofanana na yako?

Katika nchi inayoheshimu azimio la haki za binadamu ni jambo la ajabu mtu kutokuheshimu uhuru wa mtu kuzungumza!

Busara zetu na zionekane katika matendo yetu na kunena kwetu, na pale inapobidi, tupingane kwa hoja na kujenga (kushirikisha nguvu misuri ya ubongo) na si kutukana na kukashfiana.

Binafsi nimemuelewa mtoa maada! Kabainisha kuwa kuna mazuri (machache) na mabaya (mengi) katika awamu hii ya tano! Labda yuko sahihi, ila nadhani awamu hii ya tano haijatimiza hata mwaka mmoja ofisini, yawezekana ni mapema mno kutoa hukumu ya jumla.
 
Kila aliempa kura Lowasa hajuti, alifanya maamuzi sahihi kabisa na Mungu lazima atatbariki wote. Hili lichama la majambazi angalia linavyoendeleza dhuluma, kisa umeya tu, hili lichama alielichagua lazima anajuta ila hawezi jitokeza hadharani. Aibu yao milele.
 
Lowassa ni jiwe hakuna anayejutia kura yake kwa Lowassa ukisikia MTU eti anajuta ujue hakumpigia Lowassa viva Kamanda EDU
 
Acha utoto CCM Na Serikali yake kama kaisha inamzuia kwanini kufanya mikutano? Achana Na Kamanda Lowassa Kipenzi cha Watanzania
 
Naungana na mtoa mada,sijuti na sitajuta tena sitokaa nikapigia kura hicho chama cha wabaka demokrasia!!
 
Japo sikukubali, Lowassa umenifundisha mambo makubwa 08 yafuatayo...

1. Ukiwa na vision kubwa isimamie bila kujali dunia au watu wanasemaje.


uliutaka urais tangu zamani na umesimamia vision yako na hukukurupuka.Mwalimj Nyerere siku moja alisema alipopata msaada aijiuliza sana. Ukiwagawia watanzania hii pesa yote wakala wakashiba, ikiisha wataomba tena, nchi hii itajaa ombaomba kuanzia watoto hadi wazee. Ndani ya ccm akaamua nitawasomesha watoto wa masikini ili wakipata elimu watakuwa na uwezo wa kuwalisha wazazi na familia zao hadi wanakufa. kwa dunia ya sasa hii inawezekana kwa ujasiliamali, kuajiliwa, kupata fursa nje ya nchi kama una elimu bora. Hili wazo lilikufa alipoondoka madarakani. Tumepiga hatua kurudi nyuma ktk umaskini wa kutupwa na utajiri wa takwimu za kifedha. Namuona kiongozi huyu Lowassa akijaribu kuiianzisha safari hii nje ya chama dola baada ya kuikosa nafasi huyo ccm huku akiacha mabaki ya ndoto hii kwa watanzania kwa mradi uliokosa wasimamizi wa SHULE ZA KATA.

2. Unanidhamu kwa viongozi wako wa dini au neno la Mungu.

uliposhauriwa kukaa kimya uliheshimu na ukawa mnyenyekevu.

3. katika maisha lazima uwe na priority katika vision yako

umesisitiza priority yako kabla na baada ya kuhama ccm elimu elimu elimu, mpinzani wako hajawahi kusikika popote akitoa dira ya taifa. Kutoa mitazamo yake na jibu kwa matatizo ya watanznia ametokezea tu kampeni zilipoanza. Anajisifia barabara ambazo hata nchi ikiwa chini ya jeshi lenye nidhamu bado zitajengwa, ndio maana anatoa ahadi moja yenye thamani ya tillioni 44 (refer nipashe ya leo).

4. Confidentiality
hii ni sifa kubwa watanzania tunazidi kuipoteza. Leo hata watu wenye heshima wakiwasiliana wakiwastressed kidogo tu wanatangaza ili wapate umaarufu mwepesi. mfano Dr weapon, Mchngj gwjm, polpl, mnadhimu lisu n.k wewe umejua siri za serikali lakini kwa usalama wa taifa na amani unajua uongee nini na kwa wakati gani. Unajua unataka kuwatumikia watanznia wakiwa sio vilema, bila machafuko.

5. Ukizuiwa kupita mlangoni na hata dirishani Bado unaweza kung'oa bati ukatoka utimize kile unachoamini kuliko kubaki na kufa kifo cha aibu na uwezo wako ukapotea.
-- plan B katika maisha haipukiki. Umenifundisha kuna sababu ya kubadilika kama unaona uelekeo uliokuwa sio sahihi. Kubadilika huitaji mwaka ni wakti mwingine ni siku moja au saa tu ya kufanya maamuzi sahihi.

6. Ukishatolea ufafanuzi jambo unasonga mbele Muda ni Mali.
ulipojieleza kwa tido miaka hiyo kuhusu richmond ukamaliza kwa kusema the "Historia itawahukumu ".
Umeamua kuwaacha wajibishane wao wewe unaendelea na focus yako.

7. Umenifundisha kuwa ukiamua kuhitaji mambo makubwa inakubidi na wewe uwe na moyo au mapafu Makubwa ya kuvumilia mishale ya maadui wa ndani na nje. Kwa mara ya kwanza Mtu mmoja anashambuliwa Kina kona, pande kuu zote za dunia, mitandaoni, magazetini. Umeundiwa kamati ya watu zaidi ya 30 kwa mara ya kwanza katk historia ya siasa ya tanzania lakini umedumu kuwa imara.

8. Unatukanwa kuhusu afya yako, huku ukiwajua kwa undani afya za wapinzani wako. yawezekana zikawa ni mbovu kuliko hata yako. Lakini umekaa kimya maana sio sehemu ya malengo yako. Maana kuruka, KUPIGA PUSH -UPS JUKWAANI au kukimbia sio kipimo pekee cha afya bora NA SIO HITAJI LA WANZANIA WALIO KATA TAMAA NA SIASA MANENO. Baba wa taifa aliondoka airport kuelekea hospitalini uingereza akiwa anatembea akitabasamu mwenye uchangamfu lakini Mwnyz Mungu aliruhusu arudi amelala. JK alipougua wote tulimpa pole ila wewe unaonekana kama mtu unayestahili magojwa na ikibidi kifo wakati hakuna anayejua kama unaumwa .


Mambo haya yamekupa heshima sana, Hata kama ikitokea Umeshinda au kushindwa Utaingia katika kitabu cha historia ya siasa africa.

Nitakupa kura yangu kabla ya saa nne asubuhi, niakutafutia na kura nyingine zaidi ya ishirini kwa kushawishi watu kama zawadi kwako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom