Ukweli tunaoukimbia

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
12,020
Reaction score
28,582
Nimekuwa nikifatilia kwa muda baadhi ya mada ambazo zinahusu mapenzi na ukabila huku baadhi ya watu wakipinga kwamba katika jamii yetu ya leo hatupaswi kuongelea masuala ya ukabila kwenye mapenzi yetu au elimu hii Sio kweli!.

Ukabila au makabila yetu yanamchango kubwa sana kwenye tabia zetu watu wanaoolewa au kuoa leo wengi ni 27years mpaka 37years hawa watu wengi wamelelewa katika familia ambazo baba na mama ni wa kabila moja kwa sababu miaka ya 1980 watu bado waliamini katika ukabila kwa hiyo mtoto lazima atakuwa na ukabila pia hata kama wazazi ni wa kabila tofauti bado mtoto atakuwa na tabia za kabila flani nzuri na mbaya kwa sababu wazazi bado wanazo tabia za makabila yao ambazo watajitahidi watoto wazifahamu

Pia unapokuwa Dar au sehem yoyote ya dunia usijedhani kwamba Tanzania ni nchi iliyoendelea sana kiasi cha nepotism kutokuwepo hii ipo makazini na kwenye ndoa kama kawaida nakubaliwa kukosolewa ila bado naamini unapotaka kuoa au kuolewa usiache kuangalia swala la ukabila ili kumuelewa mpenzi wako na kujua namna ya kumsaidia pale anapokuwa na udhaifu kumbuka mapenzi ni kusaidia udhaifu tunaokuwa nao na Sio kuangalia strength tu.
 
Kwa miaka hii ya kisasa nadhani maombi zaidi yanahitajika katika kumpata mwenza maana ni kama hata ukiangalia kabila la mtu haisadii vile japo inaweza kuwa na maana fulani, binafsi nilioa msichana wa kisingida na kiukweli wakati namtambulisha home kidogo kulikuwa na vimiguno kwa ile dhana kuwa wana vitabia fulani fulani, lakini nikafanikiwa kuzima hiyo hoja, huu ni mwaka wa 4 maisha ni ya furaha na binti yetu mmoja.
Kaka yangu ameoa mwaka jana tarehe 27 Nov, tena binti wa kabila moja na letu, hivi ninavyoandika hapa ni kuwa jana ndio ndoa imevunjika rasmi hakuna maelewano, ndoa za miaka hii zinahitaji kuongozwa na Mungu mwenyewe maana kiubinadamu, dah!....tumekuwa wajuaji sana.
 
Kuna watu wametoka makabila yanayojulikana ni mazuri lakini wao wana tabia mbaya sana na kuna watu wametoka

makabila yanayojulikana ni mabaya lakini hao watu wana tabia nzuri hamna mfano,anyway mi kwangu nadhani kumjua mtu

familia yake wakoje ni nzuri zaidi kuliko kabila.
 
Sijasema watu wasiolewe au kuoa kabila tofauti ila unapofanya hivyo jua kwamba kuna tabia au athari za kitabai anazokuwa nazo mwenza wako na ni vema ukajiandaa kukabiliana nazo kiakili na kimwili na Sio kuingia huku ukisema huyu Sio Kama wengine siku moja aweza Fanya Kama wengine lazima ujiandae kwa hilo pia.
 
Evelyn hata huyo wa kabila lako huwa na mazuri na mabaya point yangu ni kuwa hata Kama utasema usiolewe na Manila hilo utakalokuwa umechagua jua lina tabia nzuri na mbaya jiandae kuvumilia na kuondoa dhana ya kuwa umepata malaika.
 
We we we habari za ukabila hakuna sikuiz, we angalia kama mmependana kweli basi,

makabila my foot...!
 
una maanisha tuwe na wenzi wa makabila yetu au mie kichwa ngumu?

msome hapa

"usiache kuangalia swala la ukabila ili kumuelewa mpenzi wako na kujua namna ya kumsaidia pale anapokuwa na udhaifu kumbuka mapenzi ni kusaidia udhaifu tunaokuwa nao na Sio kuangalia strength tu."
 
Angalia tabia, kabila kitu gani wewe
 
msome hapa

"usiache kuangalia swala la ukabila ili kumuelewa mpenzi wako na kujua namna ya kumsaidia pale anapokuwa na udhaifu kumbuka mapenzi ni kusaidia udhaifu tunaokuwa nao na Sio kuangalia strength tu."

ahsante kwa kunidadavulia network yangu ipo low signal hakuna kabisa...
 
Evelyn hata huyo wa kabila lako huwa na mazuri na mabaya point yangu ni kuwa hata Kama utasema usiolewe na Manila hilo utakalokuwa umechagua jua lina tabia nzuri na mbaya jiandae kuvumilia na kuondoa dhana ya kuwa umepata malaika.

Amina baba...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…