StingRay
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 503
- 628
Napenda kukupongeza sana kwa kazi nzuri unayoifanya kulijenga Taifa na kurudisha heshima ya nchi yetu iliyopotea kwa muda sasa. Ila kama kawaida katika kukusaidia wewe kiongozi mkuu wa nchi, wapo wananchi wako wengi wana siri nzito kuhusu hii nchi na mchwa walioitafuna keki na rasilimali ya Taifa bila huruma na hofu ya Mungu lakini hawana mahala pa kusemea. Watanzania hawa wakipata jukwaa/kipaza sauti cha kusemea haya nchi itabadilika kwa haraka sana. Lakini mimi binafsi naomba kukuasa yafuatayo;
Ahasante sana nimeandika haya kwa heshima ya kwamba tunachangia ukuaji wa demokrasia ya kweli lakini zaidi inclusive governance ukichkulia nchini kwetu wananchi hatuna ushiriki wa michango mpana kupitia submissions.
..................StingRay
- Fanya tafakuri nzito kuhusu mambo yanayoendelea nchini kuhusu baadhi ya viongozi wako kuhusishwa katika kashfa na udhaifu wa kimaadili ya uongozi, tetesi ni nyingi sana na kwa bahati nzuri tumeshuhudia zinaanza kama tetesi kwenye mitandao ya kijamii (hapa niwapongeze Jamiiforums kwa kuanika haya) na baadae tunaona hatua sawia imechukuliwa, hii inaonesha bado machafu ni mengi kweli na bado kuna kazi kubwa inayohitaji ujasiri na uthubutu, kwani wengi wanajificha kwenye kivuli chako,
- Fanya tafakuri nzito (ukiwa mwanadamu na ulivyotuaminisha ni kiongozi unayemwogopa Mungu) ya yale uliyotuahidi kwa kiapo kipindi cha kampeni mwaka jana 2015,
- Fanya tafakuri nzito ukiwa msomi mzuri wa kiwango cha Shahada ya Uzamivu (PhD), vyeti vyako ulivyovipata si kwa heshima bali ni kwa darasa (formal education) hata kama ni sayansi halisi, kutoka hatua moja kwenda nyingine, hadhi hii ni marais wachache sana duniani wenye sifa kama yako,
- Fanya tafakuri nzito ukiwa ni kiongozi uliyejaliwa kumbukumbu ya matukio yaliyokwishapita, hili tumia hasa kuiangalia Tanzania kutoka kipindi kimoja cha utawala kwenda kingine mpaka kwako ili uwafanyie wananchi wako yale unayoyatamani na wao wanayoyatamani katika mustakabali wa Uongozi Bora, Siasa Safi na Rasilimali Watu Bora,n.k......
- Fanya tafakuri nzito ukiwa kama mwanachama mwenye msimamo usiotetereka katikati ya chama kikongwe chenye kila aina ya makundi ya watu wenye nia nzuri na mbaya katika nyanja mbalimbamili katika Taifa letu zuri hili.
- .............yako mengi mimi naishia hapa wengine pia wataongeza kulingana na ufahamu mkubwa walionao.
Ahasante sana nimeandika haya kwa heshima ya kwamba tunachangia ukuaji wa demokrasia ya kweli lakini zaidi inclusive governance ukichkulia nchini kwetu wananchi hatuna ushiriki wa michango mpana kupitia submissions.
..................StingRay