Ukweli mtupu: Abdalah Bulembo na Anthony Diallo wajiandae kuula, waandae sherehe!

Abdalah Bulembo ...alikuwa tapeli na Mjanja Mjanja wa udalali Siku anashinda uwenyekiti ....JK alimtania ....." ...ni wewe ,? Basi Yale mambo yako ya ujanja ujanja acha ...wewe ni kiongozi Sasa "
Nasikia Magufuli Kampa Bulembo ofisi pale Ocean Rd street ...na 1 ...kama mtu wake wa siasa ....Sasa sijui kama ni personal au official ....lakini Nina Mashaka wale wasanii au wapigaji wa mjini Sasa watamtumia Bulembo
 
Kutokana na hulka aliyoionyesha rais Magufuli (simuungi mkono na sotothubutu kufanya hivyo) basi hawa watu waliokuwa na Magufuli kwenye kampeni kwa hali na mali kwa hakika hatawaangusha! Magufuli ni mlipaji mzuri wa fadhila kuliko kiongozi yeyote yule aliyemtangulia!

Amedhihirisha hilo na kwa hakika hatanii! Wito wangu kwa hawa watu ni kuwa waandae mkao wa kula! Wataula kwelikweli!

Magufuli hajawaangusha washirika wake! Amewabeba kweli kweli! Waliompigania kwenye kampeni wamepewa madonge manonomanono! Wameula baada ya jasho!

Ila wale wa upande wa pili waendelee kusaga meno! Watarajie maumivu makubwa zaidi ya haya!
kabla hujalalamika kuw mtu fulani kapendelewa kwa kuteuliwa,jiulze we pia hapo ulipo unapopatia riziki ulifka kwa juhudi zako 100% or kuna mkono wa mtu umekusogeza!
 
Tatizo Watanzania mnapenda sana ku-over estimate mambo. JPM ana udhaifu wake na chama chake ndio kabisa. Kuna watu wanafikiri JPM ndio kila kitu na ataiweza Tanzania kipindi cha uongozi wake ni kujidanganya. JPM kalelewa na ccm na anafanya kazi na CCM, utafanya kazi kwa mujibu wa desturi, kanuni na utamaduni wa ccm. Anaweza kufanikiwa kudhibiti baadhi ya mambo ambayo yalikuwa ni udhaifu wa JK lakini hataweza kudhibiti udhaifu wa ccm. Nashangaa sana CUF na Maalim Seif wana imani kubwa na JPM kuliko uhalisia. Time will tell!

Mtaelewa TU Baadaye.
 
Ni ujinga kuacha watu wenye sifa na badala yake ukateua watu eti kisa walinisaidia ktk propaganda wkt wa kampeni. Ifike mahali kiwepo chombo cha kuthibitisha teuzi zinazofanywa na mkuu wa nchi ili ku

Kwa hilo nakuunga mkono na ingefaa sana hizo teuzi zikathibitishwa na bunge na hili liwepo kwenye katiba mpya. Tatizo linakuja jinsi ya kuipata hiyo katiba mpya iliyopendekezwa na wananchi huku wabunge wengi bungeni wakiwa wa ccm na ndio hawataki kuisikia katiba ya wananchi. Anachosubiri raisi hapo ni kuchukua kile kiporo cha Sitta na kukileta kwa wananchi na kama kawaida yao wataipitisha na kumwachia raisi madaraka yake ya kifalme wakiamini ccm itaendelea kuongoza nchi hii milele.
 
maghufuli tangu mwanzo alishaonyesha hulka ya kutaka kugawa vyeo kama njugu. tusubiri tutaona mengi...
 
Ni muda sana huyu bwana hatujasikia habari zake hasa kwa huu mgawanyo wa vyeo vya shukrani kwa wale walioshirikiana na mh Rais kupiga Push Ups. kiukweli wapo wengi ambao walimsaidia kupiga push ups naye hakuwasahau akiwepo ndugu polepole ambaye alijitahidi kuonesha anapiga push ups nyingi zaidi na kutuma mpaka video kwenye mitandao akiwa tayari ameshakunywa Red Bull imsadie aweze piga push ups. naye imemlipa amepata nafasi ya kuwa mkuu wa wilaya.

wapo wengi wengi sana lakini Bwana Diallo ni kimya kirefu hajasikika kwenye medani hizi. au pengine amesaidiwa kwa namna nyingine ambayo haina haja ya kumweka public? naamini hajasaulika na Mh Dr Magufuli katika nafasi zake kama ambavyo alimwahidi kuwa naye atakuwa mahali pema duniani mara ashikapo nafasi ya Urais. Diallo alijitoa kwa hali na mali kwa kutumia vyombo vyake vya habari kuhakikisha watu wanafaham Mh Rais anapigia push up sehemu gani za Tanzania. Kwa sasa naamini Mh Anaendelea na mazoezi yake ya kupiga push ups huko ofisini kila siku asubuh au jioni.Bila shaka hajaacha tabia hiyo.

Nasikitika tu mimi sikuwa na uwezo wa kupiga push ups maana mkono wangu ulikuwa umeshtuka kidogo. who knows? pengine nami ningekuwa................... Ibarikiwa nchi yangu.
 
Kutokana na hulka aliyoionyesha rais Magufuli (simuungi mkono na sotothubutu kufanya hivyo) basi hawa watu waliokuwa na Magufuli kwenye kampeni kwa hali na mali kwa hakika hatawaangusha! Magufuli ni mlipaji mzuri wa fadhila kuliko kiongozi yeyote yule aliyemtangulia!

Amedhihirisha hilo na kwa hakika hatanii! Wito wangu kwa hawa watu ni kuwa waandae mkao wa kula! Wataula kwelikweli!

Magufuli hajawaangusha washirika wake! Amewabeba kweli kweli! Waliompigania kwenye kampeni wamepewa madonge manonomanono! Wameula baada ya jasho!

Ila wale wa upande wa pili waendelee kusaga meno! Watarajie maumivu makubwa zaidi ya haya!

Yametimia
 
Mi huwa sidharau mada za hili jukwaa.
Huna najivunia sana kuwa humu.
Watabiri wa humu mara nyingi tabiri zao huwa ni za kweli
 
Ni ujinga kuacha watu wenye sifa na badala yake ukateua watu eti kisa walinisaidia ktk propaganda wkt wa kampeni. Ifike mahali kiwepo chombo cha kuthibitisha teuzi zinazofanywa na mkuu wa nchi ili ku
Hayo mamlaka anayo na ameshayatimiza na hakuna wa kubisha
 
Back
Top Bottom