UKWELI MCHUNGU

Mkuu kwa kweli nashindwa niongee nini mana wadau tayali wameshaongea uko mwanzo, yote kwa yote nitoe tu wito kwa wazazi tujitaidi sana kwenye malezi ya watoto wetu embu tujiulize kama hali ipo hivi wakat huu je huko mbele hali itakuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NImependa namna ulivyojiuliza ... nafikiri tukipata jibu la swali lako litakuwa suruhisho.
 
Kibongobongo mtoto ni wa mama. Ki biblia mtoto ni wa baba.

Ewe mkristu soma hiyooooooo
 
Dada yangu; ina maana ulitaka nitoe mifano yote ya upotokaji wa maadili kwa vijana wetu? Mimi nilitoa kwa upande wa mabinti; nilitegemea wewe uongeze na sio kuonesha kana kwamba unawatetea. Kiujumla maadili kwa vijana yameporomoja na kinachosababisha ni malezi.
 
Nakubaliana na wewe kwenye hilo; lakini wazazi wengi wanawadekeza watoto.
Kuhusu shule zenye kazi za kujitegemea .. kama zipo labda .... sijui ...
Naangalia hapa nilipo jijini Mwanza;
Ni shule ipi yenye shamba?
Ni shule ipi yenye mradi wa nguruwe, ng'ombe, kuku n.k
Ni shule ipi ina mradi wowote ambao vijana wanaenda kujifunzia?
Nakumbuka shuleni kwetu (sekondari) kulikuwa na shamba kubwa; na bado kulikuwa na m ifugo ambapo wanafunzi tulipangiwa zamu za kuhudumia hiyo mifugo.
Tusidanganyane hiyo haipo tena.
 
Kama nimekuelewa vile.umegusa ukweli uliyopo hakika hii itakuwa Post Bora sana...
 
Umeongea kitu kikubwa sana mie naona tuache lawama za kusukumiana mzigo na familia ilelewe na wazazi wote kuepukana na majuto ya badae maana unaweza mtegemea mwanamke na ukakuta yeye anaishi kisasa so ni bora baba kama kichwa cha familia ukashika usukani wa malezi maana aibu ikurudi itawarudia watoto wa baba na mama fulani haitamwacha mtu salama
Ukweli wanawake wa sasa hivi wengi wao tunaishi maisha ya maigizo sana tunazalisha kizazi cha ajabu muhimu ni kinababa mrudi kama vichwa vya familia sio kazi kurudi nyumbani usiku mkubwa na kuondoka ( nakumbuka zamani kuna nyumba huingii ukisikia baba yao kaja kwanza anawashikisha majembe + mafyekeo ni kulima bustani huko njee kukata michongoma na kazi nyingine) tofauti na wababa wa siku hizi wakirudi anachukua watoto wanakaa kuangalia movie mara music mara game ndio ni nzuri lakini je unawafundisha kazi nyingine za nyumbani
 
Educative thread even tho' the decision of caring kids should be not to women/wives only.
 
Kama nimekuelewa vile.umegusa ukweli uliyopo hakika hii itakuwa Post Bora sana...
Tuendelee kushauriana kwa yaliyo mema badala ya kujadili yale ya sirini.
 
Ndiyo maana lawama yangu namba moja ilikuwa kwenye tech! Nimekuelewa vizuri sana Sonia G
 
Nadhani mtoa post watakao kuelewa kwa wingi ni wanawake wa mikoani,%kubwa watu wa mijini wanasingizia kazi na kukwepa majumu yao na muda mwingi wanatumia wakiwa katika mitandao ya kijamii na malezi ya watoto anaachiwa dada wa kazi,kwa hili naungana na mtoa uzi nazaidi upande was akina mama badilikeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko powa!
Wa mijini (wanawake) ukijaribu kuwatreat inavyotakiwa wanakimbilia kwenye taasisi za kutetea haki zao. Hizi taasisi zimekaa kimasilahi zaidi. Tujue wazi kwamba tunakokwenda sio kwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…