Habari zenu waungwana,
Katika hali halisi ya maisha ya mwanadamu, yamekuwa yakigubikwa na imani za aina mbali mbali.
Mimi napenda kuangalizia suala la imani ya ndoto.Kuna wengine huamini ndoto kama ndio muongozo wa maisha yao na kufuata na kutekeleza kila kile wanachokiona ndotoni.
Hili limo hasa katika zile familia za watu wanaomiliki mizimu ila kwa wengine hawana imani nazo kabisa na kuona ni kama mawazo mtu alio lala nayo.
Je, kuna ukweli gani kuhusu ndoto?