Ukweli kuhusu mshahara

Ukweli kuhusu mshahara

Pyepyepye

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2017
Posts
1,940
Reaction score
3,842
(1.) Mshahara wako hautakutajirisha. Maana bosi wako sio mpumbavu wa kiwango hicho.

(2.) Mshahara wako umepangwa ili kutosheleza mahitaji yako ya kila siku na hata ukizidi, hauwezi kukufaa kwa siku 100 zijazo. Sana sana hulautoshlezi kabisaaa.

(3.) Ikiwa kampuni yako inakupa thamani halisi ya huduma unayoitoa, ujue wanafanya kazi kwa hasara na hakuna wajiri mwehu kwa kiwango hicho.

(4.) Mara baada ya kupata ajira (HIRED), wakati wowote unaweza fukuzwa kazi (FIRED) au kustaafu (RETIRED), unaweza pia kujiuzulu wakati utapochoka (TIRED)

(5.) Mshahara ni rushwa unayopewa ili kusahau ndoto, familia, uhuru, kujiheshimu, thamani halisi ya elimu yako, maisha ya kijamii na malengo mengine binafsi.

(6.) Watoto wako hawataweza kurithi nafasi yako katika kampuni hiyo uliyoajiriwa. Ajira sio urithi. Amka kijana.

(7.) Kama mshahara wako hautoshi kulipa bili zako na mahitaji mengine mengi ya msingi na kukubakishia akiba. Yatosha sasa kujiandaa kwa umaskini baada ya kuacha kazi.

(8.) Ikiwa wewe ni mwajiriwa waza zaidi ya kula na kuvaa. Waza uzee, waza magonjwa yanayoweza kukufanya ukalala kitandani kwa muda mrefu ikiwemo kupooza. Utakapo patwa na haya utaweza tumia akiba yako na ikakufaa, je itatosha?

(9) Kuwa mfanyakazi ni sawa na kuwa mtumwa, kuwa mwajiriwa ni sawa na kuwa mke. Kwani unaishi kwa maelekezo ya bosi, wala huwezi kujiamulia tu bila ruhusa ya bosi.

(10.) Kwenye jarida la Forbes linalo ripoti watu matajir duniani, ulishawahi ona tajiri aliyeajiriwa?
Unalojambo la kuufanyia mshahara wako. Tumia mshahara wako kama ufunguo wa kukufikisha kwenye malengo yako.
 
Toa fungu la kumi uone maajabu ya mwenyezi Mungu
 
Toa fungu la kumi uone maajabu ya mwenyezi Mungu
Unapeleka kwa pale kardinali Pengo/mzee wa upako?

Bora ipelekwe straight kwny kituo cha watoto yatima,full stop.
 
Usikatishe watu tamaa.Kazi yako ya utapeli utaishia kwenye shimo la chewa.Acha wenzako watafute rizq halalan daima.

Sometimes when you get disappointment it makes you stronger
 
Kuna watu wameajiriwa wamefanya mambo makubwa sana, kuna wengine wamejiajiri wenyewe nao wako mbali mno.
Mwisho wa siku sio unapata kiasi gani, unafanyia nini kile kiasi unachokipata?
 
Kuna watu wameajiriwa wamefanya mambo makubwa sana, kuna wengine wamejiajiri wenyewe nao wako mbali mno.
Mwisho wa siku sio unapata kiasi gani, unafanyia nini kile kiasi unachokipata?
Yote kheri kuajiriwa/kujiajiri ili mradi kazi halali,umaskini na utajili ni matokeo tu
 
Back
Top Bottom