Ukweli kuhusu binadamu wa kwanza

KazidiBBM

Member
Joined
Jul 27, 2016
Posts
16
Reaction score
8
Kama binadamu wakwanza aligunduliwa kuwa alikuwa ni mtu aliyeishi bara la Africa lakini pia katika East Africa tena ni ndani ya nchi ya Tanzania ndivyo waandishi wa vitabu mbalimbali vya kidunia wasemavyo je ADAM na EVA/HAWA walikuwa wabongo?

Maoni yako au msaada wako katika hilo kulingana na jinsi unavyoelewa.

Karibu.
 
Sio kweli nadhani tafiti zaidi zinatakiwa kufanyika, kama ni kweli watanzania tusingekuwa malofa
 
Dini na sayansi haziendani.. Adam na hawa waliumbwa (watu wa kwanza) na Mungu-dini
Binadamu wa kwanza alitokana na sokwe-sayansi
 

Na aliyemgundua huyo kuwa ni wa kwanza yeye alikuwa wa ngapi?

Hapa kwenye thread yako pana Historia, Sayansi na Dini. Ngoja tusubiri wajuvi wa mambo.
 
Kilichogunduliwa ni mifupa/mabaki ya binadamu anaesadikiwa kuishi miaka mingi zaidi. Ina maana kama kuna masalia mengine hayajagunduliwa, haya yaliyogunduliwa yanaendelea kushika record.

Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kwamba hayo masalia yaliyogunduliwa ni ya Adam.
 
hapo umechanganya evolution na creation. vitu viwili ambayo ni maadui.

sasa chagua mwelekeo unaopenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…