Ukuaji wa Timu Katika Mradi na Aina ya Uongozi

The Consult

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
220
252
296b147.jpg

Kuna njia (models) mbalimbali ambazo huelezea namna timu ya mradi (project team) inavyokua (evolving). Moja ya njia maarufu (popular) ni hii yenye kuonyesha hatua nne za ukuaji wa timu, kama zinavyofafanuliwa hapa chini;
  • Forming, hii ni hatua ya kwanza kabisa katika ukuaji wa timu. Katika hatua hii wana timu (team members) hukusanya taarifa juu ya mradi; hushughulishwa na kutaka kujua; watafanya nini haswa katika mradi, nani na mwenye tabia zipi atakuwa katika timu, kwa kiasi gani wana timu wataweza kufanya kazi kwa pamoja (matching). Pia katika hatua hii wana timu hujishughulisha na kujua aina ya uongozi wa msimamizi wa mradi (project manager's leadership style)
Aina ya uongozi katika hatua hii; Katika hatua hii wana timu kwa kiasi kikubwa huhitaji taarifa juu ya maswali yanayowatatiza kutoka kwa msimamizi wa mradi (Project Manager). Hivyo ni jukumu la msimamizi wa mradi kuwaongoza wana timu katika kujua majukumu yao halisi, muundo wa mradi, malengo tarajiwa ya mradi na matarajio (expectations) ya uongozi kutoka kwa wana timu.

  • Storming; katika hatua hii wana timu huanza kufanyia kazi kile walichojifunza na kufahamu katika hatua ya forming. Katika hatua hii ndipo wana timu huweza kujua ni kwa kiasi gani wanavutiwa na malengo ya mradi husika, kwa kiasi gani wanavutiwa na aina ya uongozi wa msimamizi wa mradi, pia kwa kiasi gani wanaweza kuvumiliana wao kwa wao kitabia.
Aina ya uongozi katika hatua hii; migogoro huanza kuchipua katika hatua hii ya ukuaji wa timu, na msimamizi wa mradi hapaswi kupuuzia hata kidogo hii migogoro, hivyo msimamizi wa mradi anapaswa kuwa makini katika uongozi wake na "coaching approach" ndio hupaswa kutumika sana katika hatua hii.

  • Norming; katika hatua hii, timu ya mradi huwa tayari wamepata uelewa juu ya majukumu yao katika mradi, hivyo huanza kujikita kikamilifu katika majukumu yao. Pia katika hatua hii, wana timu huanza kufahamiana kitabia na kuanza kuwa na "spirit" ya ufanyaji kazi kwa pamoja.
Aina ya uongozi katika hatua hii; Katika hatua hii uhusika (involvement) wa msimamizi wa mradi kwa timu huanza kupungua, hii hutokana na kwamba wana timu wamekwisha anza kujikita katika kazi zao, baada ya kujua majukmu yao, pia baada ya kujuana wao kwa wao kitabia na kiutendaji.

  • Performing; Katika hatua hii wana timu huanza kufanya kazi kwa pamoja (working as a team) na kuzalisha kile kinachotarajiwa (expected results). Katika hatua hii,wana timu huanza kufanya maamuzi wenyewe, pia uwezo wao wa kutatua matatizo (problem solving skills) huongezeka.
Aina ya uongozi katika hatua hii; hii ni hatua rahisi na isiyo na majukumu mengi kwa msimamizi wa mradi husika. Katika hatua hii; kiongozi wa mradi anakuwa na uhakika juu ya uwezo wa timu ya mradi, hivyo pindi atoapo majukumu hana mashaka katika utekelezaji wake.


The Consult; +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania

Kwa huduma za;

  • Uandishi wa michanganuo ya miradi na mipango mkakati (Project Proposals & Strategic Plans)
  • Utoaji wa ushauri na semina katika Usimamizi wa Miradi na Mipango Mkakati (Project Management & Strategic Management)
Karibu
Your Success is My Desire
 
Back
Top Bottom