Ukraine yaionya Afrika kuiunga mkono Urusi katika vita

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Serikali ya Ukraine imeripoti kuwa raia 1,436 kutoka Nchi 36 Barani Afrika wamejiunga na jeshi la Urusi katika vita dhidi ya Ukraine, huku ikionya kuwa idadi halisi huenda ni kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andriy Sybiha aliyoiandika Novemba 7, 2025 kupitia ukurasa wake wa X, amesema Urusi inawashawishi Waafrika katika mikataba ya kijeshi ambayo aliifananisha na “hukumu ya kifo,” kwa maelezo kuwa wengi wao hutumwa moja kwa moja kwenye mashambulizi hatari na kuuawa haraka.

Kwa mujibu wa taarifa ya Novemba 6, 2025 iliyochapishwa na Independent Online news (IOL news) kutoka Afrika Kusini, Serikali ya Taifa hilo ilisema inachunguza kuhusu Wanaume 17 wa Taifa hilo waliokwama Ukraine baada ya kilichosemwa ni “kudanganywa na mikataba ya ajira”.

Serikali ya Afrika Kusini ilitoa tahadhari kwa Wanawake Vijana kuhusu matangazo ya uongo yanayosambazwa na watu maarufu wa Mitandaoni, wakiahidi ajira na masomo nchini Urusi, kufuatia visa vya udanganyifu vilivyogunduliwa mwaka uliopita.

Oktoba 27, 2025 chombo cha Habari nchini Kenya cha Citizen Digital, kiliandika kuwa baadhi ya raia wa Kenya walikamatwa katika kambi za Kijeshi nchini Urusi baada ya kujikuta kwenye mgogoro bila kujua, ikionesha jinsi raia wa Afrika wanavyodanganywa kuingia vitani huku juhudi za kidiplomasia zikifanyika ili kuwaondoa.

Taarifa ya chombo hicho ilieleza kuwa “Serikali imethibitisha kuwa inaendeleza juhudi za kidiplomasia kuhakikisha kuachiliwa na kurejea salama kwa Wakenya waliokwama katika operesheni za kijeshi za Urusi”.

Aidha, taarifa ya Sybiha imesema "kuna njia mbili za kuepuka hatima kama hiyo. Kwanza, msijiunge na jeshi la Urusi wala msisaini hati yoyote na mamlaka za Urusi. Natoa wito kwa serikali zote za Nchi za Afrika kuwaonya raia wao hadharani dhidi ya kujiunga na jeshi la uvamizi la Urusi,”.
1762606295128.png

==========
More than 1,400 citizens from three dozen African countries are fighting alongside Russian forces in Ukraine, Kyiv's foreign minister said on Friday.

Ukrainian officials say Russia has tried to bolster the force attacking its smaller neighbour by recruiting fighters from a variety of countries, sometimes through subterfuge.

"Foreign citizens in the Russian army have a sad fate," he wrote on X. "Most of them are immediately sent to the so-called 'meat assaults', where they are quickly killed."

South Africa said on Thursday it would investigate how 17 of its citizens joined mercenary forces after the men sent distress calls for help to return home.

And Kenya said last month that some of its citizens had been detained in military camps across Russia after unknowingly getting caught up in the conflict.

Sybiha said the total number of African recruits could be higher than the 1,436 identified, originating from 36 countries, and that most foreign mercenaries in Ukrainian custody had been captured during their first combat mission.

Source: Reuters
 
Waache kulialia! Hata wao wanasaidiwa na watu kutoka nchi zingine nyingi.
 
Back
Top Bottom