Ukraine yahimiza vikwazo vya haraka dhidi ya Urusi

Ukraine yahimiza vikwazo vya haraka dhidi ya Urusi

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewataka washirika wake kuharakisha kuiwekea Urusi vikwazo vipya baada ya Urusi kuishambulia Ukraine usiku kucha kwa kutumia makombora na mamia ya ndege za droni.

Zelensky amesema lazima shinikizo dhidi ya Urusi liwe na nguvu za kutosha ili nchi hiyo ione madhara ya ugaidi wake.

Urusi imeushambulia mji mkuu wa Ukraine, Kiyv kwa makombora 18 na droni zipatazo 400. Hayo ni mashambulizi ya pili makubwa ya Urusi dhidi ya Ukraine kuwahi kushuhudiwa mnamo siku za karibuni.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameidhinisha kupelekwa silaha za kujihami nchini Ukraine na anatafakari kuiwekea Urusi vikwazo vya ziada. Trump amesema amefadhaishwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kuhusu kuongezeka kwa vifo katika vita vyake dhidi ya Ukraine.

Wakati huo huo, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, na wa Urusi, Sergei Lavrov, watakutana nchini Malaysia.
 
Back
Top Bottom