Ukosefu wa fikra chanzo cha foleni mijini

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,428
13,936
Hata kama tukijenga barabara za juu nyingi pamoja na kuongeza barabara za magari ya kwenda haraka kama viongozi wetu na wananchi kwa ujumla hatutabadilika kifikra bado foleni haitakwisha mijini. Barabara zilizoko sasa ni nyingi na zinatosha sana ila hatuna mipango mizuri ya namna ya kuzitumia kwa mafanikio. Nichukulie Marekani ambako nina uzoefu nako kwenye hili, wao pamoja na kuwa na magari mengi kuliko sisi lakini foleni kwao sio shida saana kutokana na mambo yafuatayo ambayo hata sisi tunayaweza sana tu kama tukiamua kubadilika:

1. Njia mbadala za usafiri: Wamerekani wengi wanatumia baiskeli kwenda kazini, sokoni na safari zao nyingine fupifupi (ona picha za vituo vya baiskeli niliyoipiga kule mwaka 2012)na wana vitu
upload_2017-2-8_9-1-45.jpeg
. Pia wako wanao slide kwenda na kurudi shuleni na kwingineko.

upload_2017-2-8_9-19-54.jpeg


2. Vituo vya magari binafsi kabla ya kuingia mjini: Wametenga maeneo ya wazi mwanzoni mwa barabara zinazoingia mjini ambako wenye magari yatapark na kuyaacha huko na kuingia mjini kwa kutumia magari/treni ya usafiri yanayoanzia na kuishia pale.

3. Kupandisha kodi ya parking kwa watu binafsi: hii inapunguza hamu ya mtu kuingia mjini na gari lake binafsi

4. Kulipa kodi ya kuingia mjini: Kama unataka kuingia na gari lako hadi mjini kuna kodi kubwa utalipa palepale mwanzo wa barabara.

5. Mabasi/treni makubwa na mengi ya usafiri yaliyoratibiwa vizuri kwa muda na njia/route na za kupita na vituo vya kusimama. Vijitabu vya route, muda na vituo vinatolewa.

6. Flyovers nyingi na taa chake sana barabarani. Flyover moja au mbili tu mjini hazisaidii kitu kama mbele magari yanakokwenda hakuna flyover nyingine.

7. Kamera nyingi za barabarani zinawasaidia sana kuliko kujaza polisi barabarani

8. Misafara ya viongozi: Marekani wana viongozi wengi sana walioyoko madarakani na waliyostaafu, lakini hawafungi barabara zao au kusimamisha magari ili kupisha viongozi na wegeni maarufu wapite. Hapa kwetu hiki ni chanzo kikuu pia cha foleni

9. Watu kuendesha magari madogo tu: marekani ukubwa wa gari una determine hata gharama za kuegesha gari, watu wengi wana magari madogo/saloon. Na wanafamilia wana tabia ya kutumia gari moja kusafiria wote kwenda kazi. Hapa kwetu mke, baba, na watoto kila mtu anaingia mjini na gari lake.

10. Kuthamini usafiri wa umma. Wenzetu hata mawaziri wanajisikia fahari kutumia usafiri wa umma. Hapa kwedi looooo!!!

Kwa mwenendo huu hatufiki.
 
Mimi namiliki baiskeli lakini hapa mjini kuendesha kabaiskeli kangu ni shida ni sawa na kuhatarisha maisha maana nagombea Barbara na bodaboda na magari
 
Mimi namiliki baiskeli lakini hapa mjini kuendesha kabaiskeli kangu ni shida ni sawa na kuhatarisha maisha maana nagombea Barbara na bodaboda na magari
wenzetu wameshazoea kutii sheria kwa shuruti, kama ukiambiwa hiki hakiruhusiwi inabaki hivyo leo, kesho na hata milele
 
Back
Top Bottom