Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by vukani, Mar 19, 2010.

 1. vukani

  vukani JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nakuasa usikie, usemaji ni karama,
  Maneno usirukie, sema mambo kwa kupima,
  Utamkapo ujue, neno halirudi nyuma,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Kheri ujinyamazie, ovu huleta khasama,
  Majuto yasikujia, “Laiti nisingesema”,
  Mtu baa azuae, Motowe utamchoma,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Ni wengi wajiponzao, kwa zao mbovu kalima,
  Heshima waitakao, waseme usemi mwema,
  Wale waumbukanao, ni kwa ndimi kuparama,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Watazame wakuao, dunia kuwatazama,
  Ni wale wapimiao, kabla ya kuyasema,
  Na kimya wanyamazao, wakosapo neno jema,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Neno huenda likuwe,lizidi hata vilima,
  Mambo mawi liyazue, akili zende mrama,
  Au mema yatukie, liwapo neno la wema,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Funzo walitufunzao, wazungupule wa zama
  Zama za kale na leo, walokimcha Karima,
  Yawe mema tusemao, tusije zusha zahama,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Mola akubarikie, na ambaye akusoma,
  Na furaha ututie, uwe ni diwani njema,
  Mema utuhadithie, wana kwa watu wazima,
  Ukosapo neno jema, kheri ujinyamazie.

  Shairi hili limetungwa na Mshairi maarufu Afrika Mashariki Sheikh Amri Abedi

   
 2. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ..... Yawe mema tusemao, tusije zusha zahama,
  ukosapo neno jema, heri ujinyamazie,
  Mola akubarikie, na ambae akusoma ....
  Kweli tupu Sheikh alitanabaisha hapa.
   
 3. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,727
  Likes Received: 8,291
  Trophy Points: 280
  Vukani wampenda malenga huyu!!!!
   
Loading...