Ukoloni mpya ni mbaya kuliko ule ulowasumbua akina Milambo na Mkwawa!! what should we do?

LATTICE BOND

JF-Expert Member
May 30, 2011
219
48
Nchi za magharibi zilianza kusambaza ukoloni mpya katika mashariki ya kati na zinaelekea kufanikiwa!!
Sasa zimerudi Afrika Tayari Tunisia, Misri, Sudan na Libya wamemaliza kazi. Safari hii wanaandaa safu ya uongozi wa watu weusi kutokea hukohuko Ulaya magharibi na kuwaleta kinyemela. Hao mapandikizi tutawaona kama wenzetu kwani ni Waafrika kama sisi kumbe ni vibaraka wanaotimiza matakwa ya MABEBERU!!! tujiulize "kama wamefanikiwa kuingiza pumba miongoni mwetu, je tutaweza kuzichambua hizo pumba hasa ukizingatia hizo pumba zimechanganywa hadi kwenye uongozi na ulinzi?
should we join them or fight them?

TAFAKARI!!
 
Kinachotakiwa kwa sasa ni kila mtu mahala alipo aanze kujitazama ni namna gani ataweza kuikomboa nchi yetu kutoka kwa hawa wazungu ambao wametuandama kwa miaka mingi sana.
Maswali machache ya kujiuliza:
-Tanzania na afrika kwa ujumla ilipata uhuru wake miaka ya 60-80 kwa shida sana kutoka kwa hawa wakoloni.
-Je wakoloni waliondoka kwa mapenzi yao?
-Km waliondoka kwa mapenzi yao ni kwann waliyapata hayo mapenzi?
-Km hawakuondoka kwa mapenzi yao, je wameridhika na ile hali?
-Je k2 kikubwa kilichowaleta huku leo hakipo?

Mapendekezo yangu:
-Vijana wa sasa wa kitanzania tuondoe tamaa za kufanyia kazi matumbo yetu na kuuwaza utaifa kwanza km walivyofanya vijana wenzetu wa wakati huo nyerere, nkurumah, mandela etc.
-Tuanzishe na kujiunga ktk vikundi mbalimbali vya harakati ili badae tuweze kuviunga na kuwa na sauti moja wenye uwezo wa kusimamia umoja na uzalendo wa kitaifa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom