WanaJF!
Hii dhana ya uwajibikaji imekuwa ikipendwa sana kutumiwa na viongozi wa CHADEMA, hasa kwa viongozi wa serikali pindi taasisi wanazo zisimamia kutoleta matokeo mazuri baada ya usimamizi wao kwenye taasisi husika kuwa na madhaifu.
Kwa usikivu wa viongozi wa CCM na serikali yake, imekuwa ikishinikiza viongozi ambao wameonyesha mapungufu makubwa katika kusimamia taasisi zao, kuachia ngazi na kupisha wengine ambao wanaaminiwa kuweza kumudu taasisi hizo. Ingawa kiuhalisia si kazi nyepesi kumuondoa mtu kwenye ofisi.
Lakini napenda ifahamike kuwa, kuwajibika kwa kiongozi sio lazima yeye mwenyewe ndiye awe chanzo cha kuleta matokeo mabaya kwenye taasisi anayo isimamia, lah hasha, bali yaweza ikawa ni uzembe wa mtendaji ambae yuko chini yake, na kwa hilo tu linaweza kumuondoa kiongozi huyo kwenye nafasi yake.
Dr Slaa kama mtendaji mkuu wa CHADEMA, yeye ndiye ana wajibu wa kuzisimamia shughuli za kila siku za CHADEMA ikiwemo ulinzi na usalama wa chama. Kwa wajibu huu wa Dr Slaa, iweje mauaji yatokee kwa kiongozi wa chama huko Soweto, Arusha lakini bado tu Dr Slaa ameendelea kushikilia nafasi yake hiyo kama katibu mkuu wa CHADEMA?
Ni wazi kuwa CHADEMA ina 'intelijensia' yake, sasa kwa tukio kama lile la mlipuko uliotokea Arusha na matukio mengine yaliyo sababisha vifo, ulemavu wa kudumu na uharibifu mkubwa wa mali, kwa sababu tu ya UZEMBE wa viongozi katika kuhakikisha mikutano yao inakuwa salama, ni dhahiri kuwa Dr Slaa ana paswa awajibike kwa KUJIUZURU.
ANGALIZO;
Ndugu wanaJF, uwajibikaji wa kiongozi hauna maana ni lazima yeye ndiye awe chanzo cha kosa ama udhaifu, hapana, bali uwajibikaji ni ile hali ya kiongozi kuguswa na tukio na katika kuonyesha masikitiko yake kuhusiana na tukio zima, ndipo hapo tunakuja kwenye DHANA ya UWAJIBIKAJI.