Kitambo sana...Ilikuwa inasisimua kwa kweli, Kipindi niko shule Daah!!
Kweli vya kale ni Dhahabu.
[Chorus]
Uko wapi, Nikufuate
Niambie, Nipajue
Angalau nikuone
Roho yangu itulie.
[Verse 1.]
Najiuliza kila siku wapi pa kukutafuta,
Ni miaka mingi sana hatujaonana,,
Napata shida sana, Nataka niwe nawe
Nakupataje pataje, Nawe hauonekani
Uko wapi nieleze
Tafadhali niambie
Hata kwa barua pepe au simu ya mkononi,
Roho yangu itulie.
Repeat Chorus Again.
[Verse 2]
Moyo wangu unaniuma, Kwani kimya kimetanda.
Ningekuwa na uwezo wa kujua ulipo.
Ningekufuata huko nikujulie hali.
Niachane na mawazo ya kukuwaza wewe.
Na kukuota wewe.
Iko siku moja,moja,moja
Tutajaonana nawe..
Mimi, mimi nawee..
Repeat Chorus.
[Bridge]
Nionyeshe nikufate,
Angalau nikuone,
Nikuone, Nikuone.