kambagasa
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 2,271
- 1,809
Ni mdau wa siasa kwa muda mrefu kama mwanachama wa kawaida kwa miaka 19 sasa. Nimekuwa nachukizwa sana na tabia za wanachama kutoka vyama mbalimbali kuwageuza viongozi tuliowapa dhamana hasa madiwani na wabunge kama Saccoss zetu kwa kuwabambikia shida binafsi hususani pesa kila wanapoonekana wakiwa na shida au wakitafuta mahitaji yao.
Tatizo linakuja kuwa kubwa pale diwani ama mbuge hiyo atakapojibu hana pesa!! matusi, kupakaziwa sifa mbaya ikiwemo maringo,kujiona na kila aina ya tusi utapewa.
Tabia hii mbaya ya kujidharirisha utu wetu imeibuka kwa kadi hili kipindi kwa style ya aina yake hasa kwa waonyesha nia upande wa udiwani ambapo makundi ya jumuia mbalimbali za vyama kuwafuata au kutafuta mwakirishi kumfuata mgombea na kukuomba pesa na wakitoka hapo wanamfuata mwingine huku kadi za mialiko zikiwa na kiwango cha pesa zikimiminika kama mvua😱! tote tisa madhehebu ya dini nayo pia hayakuachi salama kwa mialiko ya uzinduzi wa kazi mbalimbali huku MC akikupamba kiunafiki ili wakukamue vizuri muda wa kutoa zawadi yako ukifika.
Hali hii imemfanya mzee wangu mmoja ndani ya chama changu kuingia kwenye mzozo na familia yake baada ya kutaka kukopa milioni nne kwa ajili ya kampeni hivyo kuweka rehani nyumba zake na mashamba hali iliyolazimu wake zake na watoto kuzua vurungu kubwa siku anawapeleka wakopeshaji kuwaonyesha hizi nyumba na mashamba pasipo hata kuwashirikisha.
Nawaombeni sana ndugu zangu tuchangue viongozi kwa kuzigatia sifa kwani tubawakatisha tamaa wale ambao hawana uwezo wa kipesa japo wana uwezo wa kutuongoza pia tunaandaa mazigira ya kuwafanya kuwa mafisadi wakijapata madaraka kwa lengo la kufidia gharama walizokuwa wanahonga.
Nawapenda sana Watanzania na hasa Watanganyika ndugu zangu muwe na siku njema.