Hajapewa dawa wala nini Mganga kacheza na Saikolojia yake tu akajua jamaa mtu wa kujirusha na kutumia. Kwa mfano kama un matumizi yafuatayo kwa vipato vya bongo jua utakua maskini. Haya tuanze;
1: Matumizi ya Bar # 50,000
2: Bajaj/Boda/Taxi # 20,00 (kwenda nakurudi)
3: Hotel ya faster room# 50,000
4: Wewe mwenyewe na washkaji na vocha # 50,000
3: Mengineyo kama mafuta ya gari yako, nakadhalika # 50,000
Kwa kadirio la chini kwa week kama itaenda vizuri utatumia sio chini ya laki mbili hadi mbili na nusu. Kwa mwezi ukigegeda mara mbili na mitoko hio hio unapata sio chini ya laki tano hadi sita.
Kazi nyingi na milioni kwa mwezi pamoja na dili za wizi unafikisha milioni mbili na kidogo. Ukitoa laki sita za matanuzi unabaki na kama milioni na nusu. Haya ipigie mahesabu ifike mwisho wa mwezi na unataka kujenga, kuwatumia nyumbani, kuwalipia ada wadogo zako. Hahahahaaaa halafu useme mganga kakupa dawa!
Badilisha tabia na mienendo yako tu. Hio salary hapo juu ukumbuke ni kadirio la juu.