Ukiondokana na uraibu wa sukari na chumvi, maisha yako utaishi kwa furaha sana sana

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,023
Reaction score
36,865
Nimeona watu wengi wanadili na pombe, ulevi kwenye uraibu.

Nikujue tu, hakuna uraibu mbaya kama wa chumvi na sukari na kutokujua vyakula vipi natakiwa kula nisipate maradhi.

Huu ni sumu inayomaliza wananchi kwa sasa, tukizika wengine watoto wadogo kabisa.

Ukienda kwa wataalamu, haya mafigo, sijui ini, sijui cancer, wengi tunaamini walevi wa pombe wanaumia sana kwenye hili, lakini kaulize Oceansroad.

Wanaoumia wengine hawajawahi hata kuonja pombe.

Kaulize wale wa figo, asilimia kubwa hawakuwahi kujua pombe mdomoni mwao.

Ndugu mpendwa ktk Bwana, wakati wa kujua sasa na kujitunza mwili wako mwenyewe.

Usipende vitu vya sukari sana wala vyenye chumvi, ukaone wajukuu wa wajukuu zako.

Ubarikiwe na Mungu wetu.
 
Hao wanaoumwa Figo wengi wao waliwekea sumu kwenye Chakula na vinywaji pasipo wao kujua.

Inabidi Kila mwezi mara Moja uwe unafanya checkup ya kiwango cha sumu mwilini kwa kufanya vipimo vyote vya Figo na ini, pasipo kusahau kufanya vipimo vya Moyo na cholesterol mwilini.

Ni hayo tu
 
tuwe wawazi tu kuwa excessive consumption ya mavitu meng sana tunayotumia ili tuishi ndio yanatupa hayo magonjwa yasiyoambukiza.

Ni muhimu kujua mwili wako unahitaj nini na nini hakihitaj kwa wingi kwa wakat uliopo. Ili kuulinda na athar za miaka 10 na kuendelea ijayo.

Kwa Mfano mtu akiwa mnene bas apunguze ulaji wa sukar(vinywaj au vyakula vyenye sukar kwa wingi) pamoja na ulaj mwing wa Wanga.

Muhim sana kila mtu ajue BMI yake. Na pia ajue nn atatakiwa apunguze na nn anatakiwa aongeze.
 
Kuhusu Pombe.
Inasababisha magonjwa meng tu kama usipoitumia kwa wastan na ukaupa mwili muda wa kurecover.

Utakuta mtu daily anakunywa maspirit.
Kula hali vizur. Halali kwa wakat.
Maji hanywi.
Utaacha kuumwa kweli?.
Uric itapanda.
utaumwa kongosho.
ukinywa maspirit na energy unaweza pata Pressure inayoenda kuharibu figo.

Ila Bia haina shida kama unakunywa kistaarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…