Ukiona mke wa mtu anakutaka jiulize (this is my story).....

KIUNGOMCHEZESHAJI

Senior Member
Oct 4, 2013
120
254
Habari za jioni wana jamvi!! Ooooh, kwa wengine inawezekana ndo asubuhi. Moja kwa amoja kwenye mada.

Ewe mwanaume!!! Ukiona mke wa mtu anakutaka kimapenzi, basi ujue kuna kitu hakiko sawa kwenye ndoa/mahusiano yake. Inawezekana ndoa yake si ndoa tena bali doa. Na anafanya hivyo kwa sababu kuu mbili; Moja, anatafuta mahali pa kupumzisha roho yake afarijike;, Sababu ya pili ni ya kiuchumi zaidi, ila hii sitaisemea sana kwa leo.

Nikitafakari katika maisha yangu tangu nianze mahusiano, nina mifano kadha wa kadha wa hili ninalosema. Mifano ni mingi ila kwa leo nitatoa mmoja. Mke wangu alipopata kazi ya kuajiriwa, aliweza kupata marafiki kazini kwake. Miongoni mwao ni dada mmoja tumuite Jackie (hypothetical name).

Walikuwa marafiki kiasi kwamba hakuna siku inapita bila kuwasiliana hata kama mmoja wao hajafika kazini siku hiyo. Wakati mwingine mke wangu alitumia simu yangu kumpigia Jackie pale simu yake ilipoishiwa vocha au charge, na wakati mwingine mke wangu akiwa kazini, kama simu yake haipatikani basi nilimpigia Jackie kuwa nahitaji kuongea naye au nilimpa ujumbe ampatie (kama ni wa haraka). Kwa kufanya hivyo Jackie na mimi kila mmoja alikuwa na namba ya mwenzake.

Baada ya muda, mawasiliano yangu na Jackie yalianza taratibu, kama mmea unavyochipua shambani, huku yeye akinitumia sms au picha au video clip ya taarifa muhimu kama vile breaking news au jambo lililo na fundisho muhimu maishani. Nilichukulia kawaida (shemeji), na mimi nikawa nafanya hivyo.

Baadaye akawa anatuma sms, picha au video za kuchekesha (jokes), baadaye akahamia kwenye jokes za mapenzi kwa design flani amazing. Nilichukulia poa, sikujali. Ikafika hatua akinitumia ananiambia nikimaliza kusoma nizifute shosti yake asije akaziona. Hapo ndipo akili yangu iliposhtuka kuwa kuna kitu hakiko sawa.

Kosa la kwanza nililofanya ni kukubali jokes zake. Zilinifanya nishindwe kumzuia asiendelea mbele zaidi. Nikawa namjibu kisanii, na kumsifia sifia kiutani zaidi. Hapo ndo nilipoharibu. Akafunguka full, kuwa ananipenda, na angependa anachopata shost yake na yeye aonje, maana inaelekea ni kitamu sana. Nilijikuta nashindwa kuzuia mafuriko, nikajikuta tunachat lakini nikiwa mwoga sana. Nilijiuliza sana , na nilimwuliza kwa nini ameamua kunipenda kiasi hiki? Mara zote akawa ananiambia tukionana ataniambia. Ikawa kila akipanga ratiba ya kuonana nakwepa, nasingizia kuwa kuna emergency au kuna kazi nimepewa kazini kwangu report inahitajika haraka kwa bosi, so tufanye siku nyingine. Siku zikaenda, wiki, mwezi, miezi. Kuna kipindi mpaka alinichukia. Baada ya muda nikaomba msamaha na kumwambia sitamwangusha tena. Siku hiyo alinitumia picha zake za uchi (alijipiga mwenyewe maziwa, mapaja na mbunye). Nilijikuta njiapanda. Baada ya muda tena mawasiliano yakapotea.

Hivi majuzi niliona profile zake fb na whatsapp kama mtu mwenye huzuni au tatizo kubwa. Nilimtafuta akawa anakwepa kuniambia. Baada ya wiki tatu ndo akaja kuniambia. Kwanza alinishushia lawama nyingi sana kwa kumtelekeza. Pili, aliniambia hayuko vizuri na mumewe kwa muda mrefu na ndo maana alikuwa akinitafuta sana maana hana pa kuweka hisia zake. Tatu, na ndicho kilichopasua jipu, ni kuwa mumewe amempa mimba msichana mwingine. Niliongea naye kwenye simu huku akiwa analia.Niko njia panda, ila nashukuru niko mbali naye kwa sasa, kuonana mpaka mtu afunge safari. Ni matumaini yangu kuwa nitavuka salama huu mtihani.

Updates!!
Kuna watu huwa ni wabishi kuamini, na wengine kufikia hatua ya kusema ni story ya kutunga. Wengine wananilaumu, anyway endeleeni kulaumu. Maana ningekuwa nimeshamgegeda huyu dada wengine bado wangelaumu. Yaani in short hatuna jema wanadamu. Mwingine amesema story haina ujumbe, sawa ni mtazamo wako but to others ina ujumbe.

Hii couple you cant imagine, kila kukicha picha zao fb hazikomi, mama yuko na hubby na mtoto wao, mara wapige picha nyumba yao, na pia mdada mwenyewe ukimwangalia alivyo mnadhifu na mzuri wa sura.... daaah, wakati mwingine naona kama they are much blessed than me, they are more happier than me, lakini kwa sasa nimeamini kuwa nyumba zinasitiri mengi. Only trust your heart. Ni hayo tuu kwa leo.
 
Hongera kwa kuishinda dhambi ya Zinaa mkuu kwani tunaambiwa tuikimbie Zinaa,La msingi Mwambie ukweli kuwa haliwezekani ubaki urafiki wa kifamilia tuu hakuna haja ya kutopeka simu zake ni Ukweli tu ndo utakuweka huru ila ukisharuhusu mazoea zaidi utashindwa kumwambia

Na wahenga wanasema hakuna Siri ya wawili ipo Siku wife ataona either Sms au picha na kukufikiria vibaya sana hatajali kuwa hamjapatana na ndipo misukosuko itaanzia hapo na wife kukosa Uaminifu na wewe

Mshauri atatue tatizo lake nyumbani na asilikimbie.
 
mwanaume halali na njaa huwa tuna chelewa kula tu naamini ipo siku tu uta mgegeda huyo dada
 
Du kweli wanaume wa mikoani mna uvumilivu.

Huku kwetu hamnaga ushemeji huyo kitambo tungekuwa tushakulaga.
 
There is no way i this word mke wa mtu atakufata na mkaanzisha mahusiano kama yuko sawa na mumewe....

Mkuu what your going through ni magumu na naelewa jinsi gan jarbu lililo ndan yako lamsingi sali sana aweke sawa mambo yake na mumewe hutamuona karibu yako tena.
 
Back
Top Bottom