Ukiona mafundi cherehani wanavyoungaunga kifaa hiki unaweza fikiria kinauzwa bei kubwa sana

Msemajiwao

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
638
1,530
Katika jambo ambalo wengi hamtalitegemea, kuna ile tape measure wanayo tumia mafundi cherehani kupimia nguo ni kwamba inauzwa Tshs 200/= tu tena rejareja, Kwa jumla inauzwa Tsh 100/=.
Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipotembea nakushuhudia mafundi wengi wanavyo hangaika na vipisi na pengine kuunganisha vipande vipande kana kwamba kinauzwa bei mbaya sana; hapo ndipo nilipogundua hawa mafundi cherehani akili zao zinafanana!!
 
IMG_20170308_174331.jpg
 
Duh! Asili ya washona nguo bongo ni wapare. Sasa hao wengine wakajikuta wanaiga utaratibu huo
 
Katika jambo ambalo wengi hamtalitegemea, kuna ile tape measure wanayo tumia mafundi cherehani kupimia nguo ni kwamba inauzwa Tshs 200/= tu tena rejareja, Kwa jumla inauzwa Tsh 100/=.
Kilichonishangaza zaidi ni pale nilipotembea nakushuhudia mafundi wengi wanavyo hangaika na vipisi na pengine kuunganisha vipande vipande kana kwamba kinauzwa bei mbaya sana; hapo ndipo nilipogundua hawa mafundi cherehani akili zao zinafanana!!

Mafundi Cherehani!

Dawa ya Mswaki!
 
Hiyo kazi ina laana ya wake za watu! Fundi siku zote hela anaperekea papuchi tu! Shillings mia kwake hasara!
KAZI YA WAPARE HIYO UNATEGEMEA NINI?
 
Inakera sana. Na wanaziungaunga ili kurahisisha wanapopima kinamama. Lazima arudie rudie ili kuhakikisha yuko sawa
 
Mda mwingine sio swala la bei... Ni mazoea na kile kitu na umetoka nacho wapi!? Kuna kipindi mama alikua anatupia tape imechooka akati hapo kwenye droo ya cherehani kuna zingine mbili tena mpyaa na pia anamiliki duka la vifaa vya ushonaji!
Ukiachana na wale wenye ubahili uliopitiliza, wengine ni mazoea tu au reason behind.
 
Najiuliza kwa nini inakuwa hivyo ...yaaani shillingi 100/200 ndio inafanya wasinunue au hali ya uchumi ndugu wajameni????

Kuna ule usemi wanasema Fundi bora ni kinyozi tu wengine wababaishaji tu
 
Hata mimi nilijua ni gharama kubwa.

Any way huenda unakuta hiyo iliyochoka ina vuta wateja
 
Back
Top Bottom