Ukikutana na mtu anayekususia deni au kitu chochote katika awamu hii huyo ni mzuri sana..

Online Pastor

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,949
2,000
Kususa hakujaanza leo.


Kama unakutana na wasusaji leo hii katika awamu hii ngumu kiuchumi,kisiasa na kijamii usijilaumu wala kujisikia vibaya.


Ebu mshukuru Mungu,cause that is a blessing in disguise.
Ukitaka kuamini kuwa ni baraka iliyojificha,ebu mkumbuke mtu kama Nabii Yona.


Nabii Yona alitumwa katika mji wa Ninawi ili awahubirie waweze mrudia Mungu,na kama watakataa basi Mungu auchome mji wote.


Na Kama haitoshi,kwa wakati ule Israeli ilikuwa chini ya utawala wa Waasyria ambao mji wao mkuu ulikuwa Ninawi.


Yaani ni kama kumtuma Manara aende kumuombea Manji msamaha mbele Magufuli ili asamehewe kashfa zake zote


Alichokifanya Yona ni kula kona kwenda Tarshishi ili Waninawi wakose Neno la Toba Mungu awaangamize.

Hata baada ya kutemwa na samaki,na kuwahubiria Waninawi bado Yona alitegemea Mungu atauangamiza mji wote na wakazi wake.


Na hata Mungu alipowasemehe Waninawi,hasira na wivu wa Yonah haukwishwa,zaidi uliongezeka.


Kuzira kwake hakukuibadilisha neema ya Mungu kwao.


TUNAJIFUNZA NINI?


Huwezi izuia riziki ya mwenzio kwa kununa.
Mungu ni wa wote,wema na wabaya hivyo tujifunze kurizika na dhawabu zake!

REFFERENCE:
Yona 4
 

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
2,687
2,000
Sijaelewa ulichoandika ila ngoja nikujibu kutokana kichwa cha habari
unajua mtu anasusia deni ni kutokana na wewe mwenyewe kutotaka kulipa kwa wakati kuleta uzungushaji ili kutaka kuzulumu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom