Mama Sabrina
JF-Expert Member
- Jul 30, 2016
- 16,620
- 27,583
Kwa wanawake/wadada mliowahi kufanya hiki kipimo cha HSG je mlifanikiwa kupata ujauzito, je kuna njia ya kupima tofauti na kipimo hiki maana kinauma sana usiku siku hiyo sikulala mpaka niliumwa homa na baada ya siku mbili nikaingia period.
Inashauriwa ukipima HSG ile ukipona tu yale maumivu ufanye ngono ili mimba iingie, sasa mimi mpenzi alikuwa mbali kiasi kwamba nilipofanyiwa nilikaa tu, mpaka leo sijawahi fanikiwa, tujuzane na kushauriana hapa ni hospitali gani nzuri, au dokta gani mzuri wa wanawake tu, nadhani hii pia itakuwa inasaidia na wengine maana uzazi kwa wengine ni mgumu sana.
Kilichofanya nikafanye hiki kipimo nilikuwa naumwa sana tumbo wakati wa hedhi, kuumwa kiuno na mbavu, lakini nilivyopima niligundulika mirija ya uzazi ina shida imevimba na ikapelekea nikawa sipati siku zangu, nilipofanyiwa kipimo hicho, hayo maumivu yaliisha kabisa maana nilichomwa sindano na dawa nikapewa, tatizo ni naona maumivu ya kuumwa wakati wa hedhi yanarudi tena yaani kiuno kinauma kama sio changu jamani.
Hebu tupeane ushauri najua wengi pia hili tatizo mnalo, najua pia kuna wataalamu humu watasaidia kutoa ushauri mzuri ili siku zijazo tulete mrejesho humu, chochote unachojua kiweke hapa maana haya maumivu ya hedhi sio mazuri kabisa pia tuelekezane sehemu nzuri zenye tiba nafuu sio kupimwa tu laki 2, dawa laki 4.
Karibuni.
ONYO: Waharibu uzi hapa hamtakiwi kabisa, usilete mada tofauti na hii.