Ukiambiwa shukran unapaswa kujibu hivi

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
4,953
6,071
Nukta muhimu ya lugha: ukiambiwa *shukran* ni makosa kurudisha neno *afwan*(nimekusamehe)
kwani hayaendani; kwamba vipi unasamehe anayekushukuru!
Sahihi mtu anapokwambia *shukran* umjibu kwa maneno mawili haya: *hubban wakarama*(kwa mapenzi na karama)
hakuna katika Lugha ya kiarabu (safi) neno afwan baada ya shukran..
hili ni kosa lililoenea kwa watu wengi, na kutengenea kwa mambo ni kutengeneza ndimi
 
Kiarabu zaidi... Basi sawa....!!!
 
pengine ni mchicha mwiba
 
Jee nikisema Shukraan Jazeelan...?
au JazzakaAllahu kheyrn?
 
Hapa sijui umenena kwa lugha hata sikuelewi
 
Bila shaka mtu alikuambia hivi. Sioni kuna lazima. Kati ya Waarabu (maarifa yangu Syria, Lebanoni, Misri) nikisema SHUKRAN wengi wao hujibu "AFWAN". Wengine husema "AHLAN" (=karibu!). Hubban wakarama sijasikia, lkn bila shaka pale huyu alyekuambia iko. Ila tu usijaribu kuweka hapa sheria kuhusu lugha.
 
Kiarabu zaidi... Basi sawa....!!!
Tatizo Nyerere alitaka Tanzania Lugha ya kiswahili itumeke kama Lugha ya taifa, ili aweze kiutawala zanzibar vizuri.

Zanzibar Ndio ilikuwa kitovu cha Lugha hii, na history ya Lugha hii, Lugha ya kiswahili ina maneno mengi ya kiarabu, kihindi, English etc..

Mkubali tu kufunzwa kiswahili..
 
Mbona pia Kiswahili kina maneno mengi ya Kibantu, hakuna sehemu inayotakiwa kujibebea umiliki wa lugha hii.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…