UKAWA tumieni mbinu hizi kushinda katazo la mikutano ya kisiasa

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,659
2,822
Kwanza nianze kwa kutoa salamu kwa wote humu ndani,ni matumaini yangu mu wazima wa afya ikizingatiwa sikukuu imepita salama salimi.

Hivi karibuni Rais Dr John Magufuli alipiga marufuku uwepo wa mikutano yahadhira ya kisiasa kwa kile alichodai ni kuwafanya watanzania kutojikita katika kazi na badala yake kupoteza muda kwa kufanya siasa badala ya kazi.

Alisema kuwa mikutano yahadhira ya kisiasa iliisha toka mwaka jana 2015 hivyo akawataka wanaotaka kufanya mikutano hiyo waifanye mwaka 2020 wakati wa uchaguzi mkuu.

Baada ya tamko hilo viongozi wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla walitoka na maazimia tofauti tofauti ya kuonyesha kutoridhika huko na tamko la Mhe Rais.wengi wakidai saual hilo lipo kikatiba (ni kweli) na wengine wakisema ni kinyume na haki za kidemokrasia katika taifa lenye mfumo wa vyama vingi(ni kweli).

Binafsi baada ya kutafakari sana nikaona bado CHADEMA na UKAWA 1 wanapaswa kuheshimu utawala uliopoa madarkani kwa maana ya kuucha ufanye kile unachokifanya kwani mwisho wa siku hakimu wa yote ni mwananchi wakati wa kupiga kura ndio ataamua nini kinampendeza katiak hayo.

Lakini 2 nikaona CHADEMA na UKAWA wanashindwa kutumia fursa za uwepo teknolojia katika kufanikisha maadhimio yao,jamani siku hizi tunaishi katika ulimwengu wa teknolijia ambayo kila mtu anauwezo wa kupata habari kulingana na vile anavyojisikia

Nakumbuka wakati wa kampeni CHADEMA walidiriki hadi kununua matangazo ya tv na redio ili kurusha mikutano yao,sasa kwa nini kipindi hiki cha kuzuia kufanya hiyo mikutano wasinunue haki za matangazo katika vituo viwili vitatu wakaenda studia akawa labda mbowe,msingwa,mbatia na lissu wakaongea na watanzania kupitia luninga tena kwa amani kabisa bila kuwepo na bugdha ya namna yeyote ile?

OK labda utasema wamiliki wa luninga wataogopa kurisha hivyo vipindi,je ni kweli inashindikanika kwa chama kikubwa kama CHADEMA kutokuwa na Redio yake hata ya online tu au tv yake hata ya online tu ambayo itatumika kwa ajili ya mambo muhimu kama hayo?

Mimi nadhani badala ya kutumia nguvu kubwa sana katika kutaka kupambana na Seriakli,wangejaribu kwanza kutumia nguvu hiyo katika kuwa na vyombo hivi vya habri ambavyo nadhani vingekuwa msaada mkubwa sana kwao katika kushinda katika baadhi ya vikwazo kutoka Serikalini hasa katika masuala yao ya umuhimu.

karibuni kwa mawazo mbadala,kejeli na matusi tusiviweke hapa kwani nina amnini vingozi wa UKAWA NA CHADEMA watakuwa wanasoma huu uzi
 
Back
Top Bottom