Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,389
- 38,667
Kuna dhana inayozua mkanganyiko kwenye kujadili mafanikio ya UKAWA na vyama vinavyounda UKAWA ambavyo ni CUF, CHADEMA,NLD NA NCCR kwa pamoja. Kuna watu wanataka kusema iliyofanikiwa ni CHADEMA dhidi ya vyama vingine vinavyounda UKAWA na siyo kwamba UKAWA imefanikiwa.
Msingi wa UKAWA kama vuguvugu la vyama vya siasa kusimamisha mgombea mmoja mmoja kwenye uchaguzi wa Mwaka 2015 kuanzia ngazi ya Udiwani, Ubunge na Urais unatokana na sheria iliyoanzisha vyama vya siasa ya mwaka 1992 ambayo inazuia vyama kuungana kwa mashirikiano maalum (alliance) badala yake vikitaka kuungana (Merging) ni lazima vyote vife na viunde chama kimoja.
Kwa mazingira kama hayo njia rahisi ni kuwa na mashirikiano yasiyo rasmi (kwa kuwa hayawezi kusajiliwa na Msajili wa vyama vya siasa) badala ya kuwa na wazo la kuungana na kuunda Muungano dhidi ya CCM. Kwa mantiki hiyo UKAWA siyo yenyewe ndiyo imeunda vyama vya siasa bali vyama vya siasa ndiyo vimeunda UKAWA.
Kama vyama vya siasa ndivyo vimeunda UKAWA bila shaka nguvu ya vyama hivyo haitokani na UKAWA bali inatokana na vyama hivyo vilivyojijenga kabla ya kuja kwa UKAWA. Ni ujinga kuuliza ni kwa nini CUF walivipa vyama vingine vinavyounda UKAWA kiti kimoja tu cha Jimbo la Kikwajuni kati ya Majimbo 54 yaliyoko Zanzibar. CUF imejijenga zaidi Zanzibar kuliko vyama vingine vyote vinavyounda UKAWA.
Kwa ivo uimara wa chama hautegemei uimara wa UKAWA ingawa ushindi wa chama unategemea sana makubaliano ndani ya UKAWA kusimamiwa ipasavyo. Changamoto kubwa iliyoko mbele ya UKAWA ni kuweza kudumu kwa kuwaelewesha wanachama wake kwamba UKAWA haijaja kuua vyama vyao wala kufanya kazi ya siasa kwa niaba ya vyama hivyo. Kila chama kinatakiwa kijijenge chenyewe ili kikija kwenye UKAWA sehemu yake kwenye keki ya UKAWA iwe kubwa.