PersonnelReporter
Member
- Dec 16, 2016
- 23
- 10
Siasa za Tanzania zina maajabu yake, maajabu ambayo hauwezi kuyakuta popote Duniani, hasa siasa za upinzani.
Kwa kumbukumbu zangu ACT WAZALENDO na UKAWA waligomea uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar uliofanyika mwezi machi mwaka jana 2016.
Madai yao ilikuwa kukiukwa kwa misingi ya demokrasia baada ya matokeo ya uchaguzi MKUU wa mwaka 2015, oktoba 25 kufutwa.
Tukio la kufutwa lilikuja kama zao la maalim SEIF kudaiwa kujitangaza kuwa mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi huo.
ZEC chini ya Jecha ilifuta matokeo na baadae kutangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi huo.
UKAWA kupitia chama cha CUF waligomea uchaguzi huo wakishinikiza kutangazwa maalim SEIF kuwa urais wa Zanzibar.
Baada ya muda mfupi ACT WAZALENDO nao wakagomea kushiriki uchaguzi huo wakitoa tamko kupitia halmashauri kuu ya chama hicho na kutaka Maalim SEIF atangazwe kuwa rais.
UKAWA NA ACT WAZALENDO walisimamia maneno yao na kugomea uchaguzi ule wa mwezi machi 2016.
Katika uchaguzi ule wa marudio hakuwepo mgombea wa UKAWA wala ACT katika ngazi yoyote kuanzia udiwani, uwakirishi wala urais.
Ni dhahiri chanzo cha mgogoro ule ilikuwa ni tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Ninachokifahamu Mimi hakuna marekebisho ya maana ya kiuongozi yaliyofanyika ndani ya ZEC mpaka kuwa wasafi wa kuaminiwa kuwa hawawezi kugufuta MATOKEO ya uchaguzi mdogo wa Dimani.
Cha ajabu ni UKAWA na ACT wale wale wameshiriki uchaguzi unao andaliwa na ZEC ile ile.
Swali kwa UKAWA na ACT WAZALENDO.
Kushiriki kwenu uchaguzi mdogo wa dimani haiwezi kuwa sababu ya kuiaminisha Dunia kuwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wake hakuna ukiukwaji wa Misingi ya Demokrasia?
ZEC imefanyiwa mabadiriko?
Hamuoni kushiriki kwenu kwenye uchaguzi wa Dimani ni rasmi mmemtambua DR. SHEIN kuwa rais halali wa Zanzibar kwani alitangazwa na ZEC inayoandaa na bila tone la shaka itamtangaza mshindi wa Dimani?
Nipeni majibu.