UKAWA mnatuchanganya, acheni sifa

Lini vocha anasaini Kinana ili muanze kuzunguka nchi nzima kama UKAWA. Je mna watu wa kuvuta watu au ni Kinana, Mwigulu na swahiba wangu Kikwete. Ila fisi wenu hawana mvuto kwetu sasa hivi tumeshawazoea, kutupakia kwenye malori hatutaki tena ajali zimezidi.

Washauri wasije wakarogwa wakaaenda na agenda ya katiba pendekezwa kwa wananchi, WATAJIMALIZA kabla ya uchaguzi
.


 

Akipata nauli huyu anakuja mjini..
 

Attachments

  • 1430328183815.jpg
    43.5 KB · Views: 130
Fuso zitapata pesa safari hii. Kusomba watu wa CCM mikoa yote si kazi ya kitoto

Nimeshanunua fuso kwa ajili ya tenda hizo mwaka huu. Mwaka 2010 tenda hizi za CCM zilimtoa sana mshkaji wangu.
 
Tunawakaribisha mtaani, ila mje na takrima ya kutosha - sisi tutajipanga tujae kwenye mikutano yenu, msisahau usafiri wa kwenda na kurudi mikutanoni, Posho za siku, ikiwezekana Pilau na Soda!! Msibadililke - Tunawasubiri kwa hamu.
pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali
 
Ukimfutilia sana mzee tupa tupa huwezi sema ni mwana-CCM na halikadhalika si mpinzani.Ana sifa zote za kuitwa kinyonga.
Hapana mkuu, wewe kweli huwa humuelewi, mbona kila akipost huwa anaandika pale chini kuwa yeye ni mzee tupatupa wa Lumumba?Inamaana mkuu wewe hujui mtaa wa Lumumba kuna ofisi za chama gani?!Haya.., hata kama hujui basi, amesema sasa kuwa UKAWA wanasababisha wao(CCM)hawali wala hawalali, na kwamba UKAWA waache sifa kwani hata wao CCM wanajipanga kujibu mapigo, bado tu hujaelewa VUTA-NKUVUTE yuko chama gani?!, masihala hayo mkuu!!
 
Last edited by a moderator:

Mzee Tupatupa nyie simpo busy kuwafundisha walimu jinsi ya kuiba kura! Kweli maji yamezidi unga.hamsha hamsha
 
Sasa nyinyi ukawa endeleeni tu yupo mbugani huku Serengeti na wengine tumewatuma gombe kuleta sokwe wekundu tukirudi full vivutio mtajaa tu nyie ukawa fisi tumeona mmewazoea
 

Anyway,sawa.
 
Last edited by a moderator:

Majimbo tisa kati ya miambili yana mgogoro ndani ya ukawa-Tundu lissu
 
Kinyume chake majimbo mia mbili ndiyo yana mgogoro NLD wanataka majimbo mia.

Teh Teh juzi CUF na Chadema waligongana Mtwara na nina sikia CUF wanataka jimbo la mtwara na Chadema wana litaka! Kwenye vikao Cuf wamegoma kushiriki hawataki kusikia kabisa! Jana Lipumba na Lissu wali hutubia kila mtu mtaa wake mmoja alikuwa mikindani na mwingine alikuwa mtwara mjini..kumbe walishindwa kuhutubia pamoja kutokana mgogoro mkubwa kuhusu jimbo la mtwara mjini!
 
Safari iliyopita mlitumia fisi kukusanya watu. Safari hii mnatarajia kuja na mbinu ipi???
 
Sasa hivi CCM mtalia na kwenda kutusemea kwa Mangu na Jaji Mutungi awaokoe.

Na manati tumeshatengeneza ya kutosha.kazi yetu sasa ni kufundisha vijana jinsi ya kutumia maana vijana wa sasa hawajui jinsi ya kulenga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…