UKAWA mmetegwa, mmetegeka, mnazama

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,169
1,073
Kila jambo linalofanywa kisiasa na wanasiasa katika ulingo wa majukumu/kazi za kisiasa lina sababu za kimkakati na mahsusi kiitikadi/msimamo/dira/mwelekeo.Haya yote hutendeka yakihusisha usahihishaji wa makosa/mapungufu/madhaifu yaliosababisha madhara/kufifia kisiasa kati ya chama kilichoshika hatamu dhidi ya vyama vyenye kiu ya kushika hatamu.

Hekima na maono vyatakiwa sana ndani ya mioyo na fahamu za viongozi wa vyama vya upinzani.Msipojitathmini /Msipojitafakari na kujitambua kwa kujirekebisha mliponena/tenda na fikiri kwa ukosefu yapo madhara makubwa ya matendo,maneno, na fikra zenu.

Vyama vya siasa vyapaswa kuwa makini na kutathmini kwa jicho la saba mipango mikakati/maono/makusudi katika teuzi za upande wa pili,mbinu za kufanikisha mambo magumu kuwa mepesi.Kuruka viunzi vya utekelezaji wa sera,ilani,rasimu n.k.

Kwa imani kubwa ambayo wananchi wameionyesha kwa vyama vinavyounda UKAWA,hamna budi kuwa na mikakati ya hekima,busara,umakini,unyoofu,kina,ubora kufikia malengo makuu ya uwepo wenu pasipo kutoka katika mikikimikiki rasmi kwa mbinu zisizo na tija chanya kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom