UKAWA: CCM wajiandae kwa anguko 2015

UKAWA: CCM wajiandae kwa anguko 2015

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930
Zanzibar.

Viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Zanzibar wameibeza ripoti iliyotolewa wiki hii na Taasisi ya Twaweza, wakisema haielezi hali halisi ilivyo.


Wamesema kwamba kutokana na ukweli huo, CCM iwe tayari kupokea matokeo magumu ya anguko katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Tamko hilo limetolewa na viongozi wa vyama vinavyounda umoja huo, walipozungumza gazeti hili kwa nyakati tofauti, kufuatia ripoti ya utafiti ya Twaweza, inayoonyesha kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anaongoza kati ya wagombea wanaotajwa kama uchaguzi ungefanyika sasa.

Makamu mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi Haji Ambari Khamis alisema kwamba muungano huo unakwenda na ajenda tatu katika kampeni za Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Alizitaja ajenda hizo kuwa ni pamoja na tatizo la umaskini, kudhrauriwa kwa Katiba ya wananchi, kuongezeka rushwa na ufisadi hali inayoathiri wananchi wa pande zote mbili za muungano.

"Kama mipango na mikakati itakwenda bila ya kujitokeza mabadiliko, CCM watakuwa na wakati mgumu kwa nafasi zote za wagombea ikiwemo urais wa Muungano na Zanzibar," alisema Ambari ambaye pia aligombea urais wa Zanzibar mwaka 2010.

Upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Zanzibar (Chadema), Said Issa Mohamed alisema kuwa Ripoti ya Twaweza inapotosha ukweli dhidi ya nguvu za Ukawa katika kuelekea uchaguzi wa mwakani.

Alisema kwamba kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Ukawa tangu kuasisiwa ni wakati mwafaka kwa viongozi na wanachama wa CCM kuanza kujitayarisha kisaikolojia ili kukubali matokeo magumu yatakayowakumba mwakani.

Hata hivyo, alisema katika ripoti hiyo kuna mambo ya msingi wanayokubaliana nayo ikiwamo kuongezeka kwa umaskini uliofikia asilimia 63 kutoka 49.

Pia, alitaja kuongezeka kwa matatizo ya huduma za afya pamoja na kuporomoka sekta ya elimu hadi kufikia asilimia 38 kutoka 46 mwaka 2012.

Alisema iwapo kuna asilimia 33 ya wananchi hawajaamua wampigie kura mgombea yeyote kwa mujibu wa ripoti hiyo, Ukawa inaamini watu hao watakuwa wamepata msimamo huo kutokana na kazi inayoendelea kufanywa na Ukawa ya kutoa elimu ya uraia kuhusu kasoro za Katiba Inayopendekezwa na sababu za kuongezeka umaskini nchini.

Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani Abdalla alisema kuwa utafiti wa Twaweza una kasoro nyingi, licha ya kueleza matatizo ya umaskini na kuanguka kwa sekta muhimu za huduma za jamii.


Alisema kuwa Twaweza imeshindwa kueleza sababu za kuongezeka kwa umaskini wakati taifa linakabiliwa na tatizo la rushwa na ufisadi.

Alisema kwamba ni kweli Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ana mvuto na kukubalika kwa wananchi wa pande mbili za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kati ya wagombea wanaotajwa wa CCM, lakini bado kikwazo kikubwa kipo ndani ya chama chake.

Alieleza kuwa iwapo Lowassa hatapitishwa kuwa mgombea wa nafasi ya urais, anguko litamkuta mgombea yoyote wa CCM kutoka kwa mgombea wa muungano wa Ukawa.

"Ripoti ya Twaweza sawa na hawawezi kwa sababu wanashindwa kusema ukweli kuhusu nguvu za Ukawa wakihofia masilahi yao," alisema Bimani.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa ni mapema kuzungumzia Ripoti ya Twaweza kwa sababu chama chake hakijakaa na kuichambua.

"Kama chama, bado hatujakaa kutathimini Ripoti ya Twaweza, lakini kabla ya matokeo ya ripoti, CCM tunajua tunashinda Tanzania Bara na Zanzibar katika uchaguzi wa mwakani," alisema Vuai.

Alisema kwamba sababu kubwa ya kushinda katika uchaguzi huo ni Serikali ya CCM kufanya vizuri katika utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Ukawa: CCM wajiandae kwa anguko 2015 - Kitaifa - mwananchi.co.tz


 
Chama tawala cha ccm kimezidi kupoteza matumaini kwa watanzia mpaka sasa kuamua kukisusa na kuamua kuchagua viongozi wa vyama vya upinzani katika chaguzi ndogo tofauti na ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita,,, hiyo ni ishara tosha kwamba mpaka kufikia uchaguzi mkuu 2015 , ccm itakuwa imefutika katika mioyo ya watanzania
 
ccm wajilaumu mwenyewe kwa kuwa na kiburi
 
Waanguke tu nimeshawachoka. Mijitu migumu utafikiri sijui nini vile!!!!u
 
tuseme inshaalah...lakini nakupa nagalizo kuwa kukwanyuka kwa tawi sio anguko la mti.. ninyi kwa umoja wenu hamjafikisha asilimia 40 ya kura zote , sisi peke yetu tumevuka asilimia 50 sasa hizo ndoto zako za mchana unaziotea mchangani wakati ukilivuta ganja?
Chama tawala cha ccm kimezidi kupoteza matumaini kwa watanzia mpaka sasa kuamua kukisusa na kuamua kuchagua viongozi wa vyama vya upinzani katika chaguzi ndogo tofauti na ilivyokuwa katika chaguzi zilizopita,,, hiyo ni ishara tosha kwamba mpaka kufikia uchaguzi mkuu 2015 , ccm itakuwa imefutika katika mioyo ya watanzania
 
Sasa ni wazi kuwa Rais Kikwete amelifikisha taifa pabaya....Tafsiri nyepesi ni kuwa utawala wa Kikwete umerahisisha zaidi harakati za kuiondosha CCM madarakani!!Wachambuzi wengi wameshachambua na bado wengine wataendelea kufanya hivyo. Wanaweza kutofautiana kwenye uwasilishaji lakini maudhui makuu (ukiacha mapungufu ya kikatiba) yanabaki kuwa pale pale kuwa kuna udhaifu mkubwa sana kwenye taasisi ya Urais! Ni rais huyu huyu aliyeweza kuwasamee wezi wa EPA, Richmond..... Ni Kikwete huyu huyu aliyewaomba wananchi kumtajia majina ya majambazi, wauza unga na wanaofanya biashara ya viungo vya albino... Ni Kikwete huyu huyu; Rais na Mwenyekiti wa CCM aliyedai anawafahamu majangili wote nchini.... Haya na mengine mengi yamelitia aibu taifa... Na vile vile ni kitanzi kwa CCM..Maamuzi dhidi ya Tibaijuka yamedhihirisha kuwa kila mtu ana mdhaifu wake.... Kila mtu anamshughulikia au kumwonea mdhaifu wake... Udhaifu huu unaweza kuchukua taswira nyingi kuanzia jinsia/jinsi, muonekano, n.k.. Kikwete kaonesha njia..... shime shime watanzania; wakati umefika wa kuiwajibisha CCM.... Sisi tuna nguvu kuliko CCM... Kumbukeni: Hatuiwajibishi CCM kwa sababu ya jina lake... Tuungane kuiwajibisha kwa sababu ya mifumo yake mibovu inayotupatia viongozi wabovu na mwisho kuwa na taifa bovu!!Kipimo cha akili yetu na uwezo wa kujiletea maendeleo hupimwa kwa jinsi tunavyotatua matatizo yetu!! CCM ni tatizo kwa maendeleo ya Tanzania!!
 
Escrow ni pesa za campain mwaka kesho hamna ubishi, ila kama kawa... Kula CCM kura Ukawa.... au kula ccm na kulala ukawa...
 
Watanzania ambao hadi leo wanaipigia kura CCM nawaona kama mataahira hivi!
 
Haya MSALANI na mmeo LAKI SI PESA, karibuni hapa mmwage uharo wenu!
 
Asalaamu ndgu zangu,
ilizoe kuongoza nchi kwamazoea.na hata matamko ya kwenye jukwaa. Kwa mfano huku kwetu CCM walikuwa wakipanda jukwani kuwanadi wagombea wao wenyeviti, walikuwa wanatukana wapinzani kana kwamba ndo sela. Hawakuweza kupata wananchi wakuwaunga mkono na kutishia kuwa CHADEMA hawana ofisi hoja ambayo ni ndogo sana. Walikuwa wanafananisha na miaka ya 2000 imekula kwao. 2015 tuchukue madiwani wabunge na raisi uchaguzi ukiwa huru magamba mchana kweupe wanag'oka
 
dr slaa alishasema ccm ni wepesi kama karatasi bila nguvu ya dola saa mbili asubuhi watu wanasherekea ushindi wa ukawa 2015
 
Unaweza kuwa na hoja nzuri, lakini kukosekana kwa usanifu wa uandishi kunaweza kuifanya hoja tako isieleweke na hatimae ukadharaulika kama hivi
 
Kwa jinsi ambavyo uchaguzi wa serekali za mitaa ulivyoenda Ni kweli CCM inaweza ikapigwa mwakani.Kuna maeneo ambayo huwezi kutegemea kuwa wapinzani hawezi kushinda lakini safari hii wamewaza kushinda.wameenda mbaliza zaidi hadi kwenye vitongoji vilivyoko mbali zaidi na vijiji ambako ndiko yaliko maficho makuu ya CCM nako wamefanikiwa kuwachomoa Kama kumchomoa panya ndani ya handaki lake.
 
Watanzania ambao hadi leo wanaipigia kura CCM nawaona kama mataahira hivi!

mkuu mbona unanishangaza? yaani wewe bado unachagua kwa kuangalia chama na si busara na elimu ya mtu? kwahiyo hata kama ni mbulula akiwa wa chama tofauti na CCM unampa kura yako. pole sana, nyie ndio mnatupeleka katika karne ya wabunge wasio na hoja bungeni.
 
Kama tutafuata vyama na sio kwa kuangalia umakini na busara basi chama kimoja kitashika hatamu. Lakini kwa wazo langu mie tujaribu kuchagua viongozi bora nasio kwa kuangalia chama.
 
tuseme inshaalah...lakini nakupa nagalizo kuwa kukwanyuka kwa tawi sio anguko la mti.. ninyi kwa umoja wenu hamjafikisha asilimia 40 ya kura zote , sisi peke yetu tumevuka asilimia 50 sasa hizo ndoto zako za mchana unaziotea mchangani wakati ukilivuta ganja?

kajifunzeni kwanza hesabu za sehemu na asilimia, msiwahadae wananchi na data zenu za kupika, eti zaidi ya 50% za tamisemi ya ccm, urojo, upuuz mtupu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom