General Mangi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 15,303
- 23,055
Wanabodi salaam
Kama tunavyoona kasi ya rais Magufuli na jinsi alivyoiteka audience katika nchi.
Kila nikitazama vyama vya upinzani hasa vilivyo katika umoja wao, UKAWA bado naona hawajui wafanye nini kwasasa.
Jinachonichanganya zaidi, Ukawa hufanya maamuzi ambayo wanashindwa kujua hatma ya maamuzi yao pale itakapo shindikana.
Kwa mfano, wameshindwa kabisa kwa umoja wao kulisimamia suala la zanzibar, wamekuwa wakitoa matamko ambayo hayana impacts yoyote kwa wafuasi wao. Ukawa kwa umoja wao wameshindwa kabisa kuwaaunganisha wafuasi wao kuamini kile wao wanaona ni sahihi.
Tukio jingine ni lile la bungeni kuhusu TBC kuonyesha matangazo live. Ukawa walitoka nje kupinga maamuzi hayo, alafu tunawaona kesho yake wapo bungeni kushiriki vikao vya bunge na kuachana na msimamo wao.
Nashindwa kuelewa wakati wanafanya maamuzi haya huwa hawajiulizi fate ya maamuzi yao itakuwa nini.
Ukawa kwa umoja wao anashindwa kuwa wabunifu wakufanya wananchi waaunge mkono.
Inashangaza Chadema kutumia rasilimali nyingi kuzunguka na helkopta nchi nzima wakati walikuwa na uwezo wakufubgua redio yao na gazeti lao na kuwafikia watanzania kila siku,kitu ambacho si tu kujitangaza, pia kupata mapato ya kukijenga chama zaidi.
Tunaweza kuwabeza CCM na vyombo vyao vya habari, lkn tukumbuke kuwa vyombo hivyo huvitangaza chama chao.
Chadema kinajua kuwa vijana wengi hata kwenye mitandao wanawaunga mkono, lakini cha kushangaza wameshindwa kutumia fursa hiyo kujiendelezaa.
Ushauri.
2. Sasa ni wakati wa kubadilika kulingana na siasa zinavyokwenda. Ni wakati wa kuweka maslai yenu pembeni na kujenga umoja, chama kamili, chama kikubwa cha upinzani, tena mushirikishe na ACT -wazalendo.
2. Mje na itikadi inayopendwa na watanzania, mfumo gani mtakao tumia kuongoza nchi.
3. Anzisheni media yenu ambayo itawafikia watanzania kujitangaza zaidi. Muunganiko wa vyama vyenu vya upinzani bungeni na kuunda chama kimoja sidhani kama mtashindwa kuwa na redio na gazeti lenu.
4. Angalieni jinsi ya kuwaunganisha watanzania wawaunge mkono pale mnapoona mnachokisimamia kinafaa kwa jamii. Inashangaza kila jambo bovu hapa nchini linafanyika lkn wananchi hawaoneshi hisia zozote kupinga ubovu huo, hapa inaonesha vyama vya upinzani mmeshindwa kuwaunganisha watantania.
5.Onesheni mifano ya kupambana na ufisadi katika majimbo yenu, kila mbunge aishi jimboni kwake na wananchi wake kutatua kero za wananchi.
Hitimisho.
Ndugu wana JF, linapokuja suala la kukosoa upinzani pale ambapo unaona si sawa, ni vema kila mtu akaunga mkono. Kama wana Ukawa mnavyopenda kuikosoa serikali ya ccm, basi na ninyi mkubali kukosolewaa.
Ifike hatua pale ambapo, Mbowe, Lissu, Lowassa, Seif, Mbatia, Zitto anakosea, tumwambie ukweli kwamba unakosea, unaharibu.
Lakini hili suala la kuwatetea kwa kila jambo linawafanya vipofu, wanabweteka zaidi.
Bado ninaimani na upinzani katika nchi yetu, lakini nataka upinzani makini na wenye nguvu ya ushawishi.
Asanteni.